Mwenyekiti
wa Timu ya Bunge (Bunge Sports Club), Mhe. William Ngeleja akizungumza
na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena Jijini Dar es
salaam leo kuhusu mechi kati ya wabunge ambao ni wapenzi wa timu ya
Simba na wapenzi wa timu ya Yanga yenye lengo la kuchangisha fedha kwa
ajili ya kusaidia wahanga wa Tetemeko la Ardhi, lililoukumba Mkoa wa
Kagera hivi karibuni. Mchezo huo utafanyika kesho kwenye Uwanja wa
Taifa, Jijini Dar es salaam. Kabla ya Mchezo huo, kutakuwa na michezo ya
Utangulizi ambapo Timu ya Bunge ya Mchezo wa Pete (Netball) inakutana
na Timu ya TBC huku Mchezo mwingine ukiwa ni ni kati ya Wasanii wa Bongo
Movie na Bongo Fleva. Mh. Ngeleja amewataka Watanzania kutoka maeneo yote nchini kujitokeza kwa wingi ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwasaidia wahanga wa Tetemeko la Ardhi Mkoani Kagera.
Mkurugenzi
wa Michezo wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Alex
Nkeyenge akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Hoteli ya
Serena Jijini Dar es salaam leo kuhusu mechi kati ya wabunge ambao ni
wapenzi wa timu ya Simba na wapenzi wa timu ya Yanga yenye lengo la
kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wahanga wa Tetemeko la Ardhi,
lililoukumba Mkoa wa Kagera hivi karibuni. Nkeyenge amewataka wale wote
watakaojitokeza kwenda kuangalia mchezo huo, wanatakiwa kuwa na tiketi
za Kielekroniki ambazo zitaanza kutumika rasmi kuanzia hiyo kesho, Pia
amezungumzia hali ya usalama katika Uwanja huo kuwa itaimarishwa vizuri
kwani Jeshi la Polisi limejipanga vyema kuhakikisha hatuna tukio lolote
la uvunjifu wa amani litakalojitokeza uwanjani hapo.
Mwenyekiti
wa Timu ya Bunge (Bunge Sports Club), Mhe. William Ngeleja akionyesha
moja ya vikombe vitakavyokabidhiwa kwa timu zitakazoshinda katika
michezo hiyo ya kesho.
Mwenyekiti
wa Timu ya Bunge (Bunge Sports Club), Mhe. William Ngeleja akipokea
mfano wa Hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 10, kutoka kwa Mtendaji
Mkuu wa Kampuni ya Mwananchi Communication LTD, Francis Nanai ikiwa ni
sehemu ya Mchango wao katika kufanikisha zoezi hilo.
Mwenyekiti
wa Timu ya Bunge (Bunge Sports Club), Mhe. William Ngeleja akipokea
mfano wa Hundi yenye thamani ya shilingi Milioni tano, kutoka kwa Kaimu
Mkurugenzi wa Tathmini ya Uhai Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),
Baraka Maduhu ikiwa ni sehemu ya Mchango wao katika kufanikisha zoezi
hilo.
Mwenyekiti
wa Timu ya Bunge (Bunge Sports Club), Mhe. William Ngeleja akipokea
mfano wa Hundi yenye thamani ya shilingi Milioni tano, kutoka kwa
mwakilishi wa Kampuni ya Jubilee Insurance.
Mwenyekiti wa Bunge, Mh. Mussa Azzan Zungu akitoa shukrani kwa niaba ya Bunge kwa wale wote waliojitoa kufanikisha zoezi hilo.
WAKATI
tiketi za elekroniki zitaanza kujaribio welo, Makampuni mbali mbali
wamechangia jumla ya Sh milioni 20 kwa ajili ya kudhamini mchezo wa
wabunge mashabiki wa Yanga na wale wa Simba utakaofanyika leo kwenye
uwanja wa Taifa ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atakuwa mgeni rasmi.
Makampuni
hayo ni Mwananchi Communication iliyotoa Sh milioni 20, mfuko wa bima
ya afya NHIF na Jubilee Insurance ambazo zote zimetoa Sh milioni 5 kila
mmoja.
Akizungumza
na Waandishi wa habari leo, Mwenyekiti wa Klabu ya Michezo ya Bunge
William Ngeleja ambaye pia ni mnazi wa Simba alisema matokeo ya mchezo
wa kesho ni hishara ya matokeo ya mchezo wa Oktoba Mosi.
Nae
Meneja Miradi wa Kampuni ya Selcom ambayo ndiyo iliyopewa jukumu la
kusimamia mfumo huo, Gallus Runyeta amesema kadi hizo zitatolewa bure
katika mchezo wa leo ikiwa ni majaribio na kuangalia dosari ambazo
zitajitokeza kabla ya kuanza kuzitumia rasmi.
Akizungumzia
jinsi ya kuitumia kadi hiyo, Runyeta alisema “Utajisajili kwa kupiga
*150*50# halafu ni lazima uiwekee pesa kwa Airtel au M-Pesa. Kiwango cha
chini cha kuongeza salio ni Sh 1,000….: “ “Unaweza ukanunua mechi moja
kwa kuandika tarehe na mchezo husika au ukachagua baadhi ya mechi au
ukanunua mechi zote za msimu za timu unayoipenda.
“Unapokwenda
kuingia uwanjani, utaweka kadi yako kwenye alama husika na mlango
utafunguka wenyewe. Ukishaangalia mechi uliyoinunua, hauwezi kesho yake
ukaenda kutazama mechi nyingine ambayo hujailipia. Kadi itasoma kwenye
mechi zilizolipiwa tu. Ukiingia uwanjani hauwezi ukatoka halafu ukarudi
kwa tiketi ileile.
Viingilio
vya mchezo huo utakuwa ni shilingi 3000 kwa mzunguko kijani na bluu,
10000 na 15000 kwa viti vya machungwa, VIP A 200,000, VIP B 100,000 na
VIP C ni 50,000 huku kutakuwa na viti 50 vilivyotengwa ambapo kwa
yoyote atakayekaa hapo atalipia 1,000,000.
Katika
mchezo huo mbali na wabunge pia kutakuwa na mechi ya bongo movie na
bongo fleva ambapo kikosi cha bongo movie kitaongozwa na King Majuto, Dr
Cheni, Check Budi, Muhogo Mchungu na Ray Kigosi wakati kwa upande wa
Bongo Fleva kitaongozwa na Rich One, Kalla Pina, Ally Kiba, Stamina, KR
Muller na H baba.
0 maoni:
Post a Comment