Saturday, September 24, 2016



Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akikatiza katika Mtaa wa Hamugembe mjini Bukoba alipokwenda kuwafariji waathirika wa tetemeko la ardhi liliua watu 17 na kujeruhi wengine 252 hivi karibuni. Picha na Phinias Bashaya

Bukoba.
Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa amewasili mjini Bukoba mkoani Kagera kuwafariji waathirika wa tetemeko la ardhi lililoukumba mkoa huo na kuua watu 17 na kujeruhi wengine 253.

Baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Bukoba, Lowassa alilakiwa na mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare na kwenda moja kwa moja katika mitaa ya Hamugembe na Kashai kuwasalimia wananchi.

Akizungumza na wananchi hao, amesema amekwenda kuwafariji na kuwaunga mkono na kwamba anataka haki itendeke kwa waathirika hao. Lowassa aliyeambatana na mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na kada wa chama hicho, Khamis Mgeja amesema atawasilisha msaada aliokwenda nao kwa mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu.MWANANCHI

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog