Saturday, July 2, 2016



Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, ajira, vijana na wenye ulemavu), Jenista Mhagama, (kulia), akizungumza jambo wakati alipotembelea banda la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwenye maonyesho ya 40 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Julai 2, 2016. Kulia ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Fulgence Sebera.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama, (katikati), akizungumza jambo wakati alipotembelea banda la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwenye maonyesho ya 40 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Julai 2, 2016. Kulia ni Afisa Uhusiano wa WCF, Zaria Mmanga, na kushoto ni Mhasibu wa Mfuko huo, Grace Tarimo

NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama, ameutaka Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), kujiweka tayari kulipa mafao ya Fidia kwa Wafanyakazi kama ambavyo Sheria ilivyoelekeza.Waziri Mhagama aliyasema hayo leo Julai 2, 2016 wakati alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea Mifuko ya Hifadhi ya Jamii inayoshiriki kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Mifuko ya Hifadhi ya Jamii iko chini ya Ofisi yake.

“Najua mnatakiwa kuanza kulipa fidia mwezi huu wa Julai, vipi mko tayari na kama bado basi mjiweke tayari kufanya hivyo.” Alisema Waziri.

Akimjibu Waziri Mhagama ambaye alifuatana na maafisa wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, (SSRA), wakiongozwa na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka hiyo, Sarah Kibonde Msika, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Fulgence Sebera alimwambia Waziri kuwa Mfuko umejiandaa kikamilifu kutoa fidia kwa wafanyakazi ambapo elimu ilitolewa kwa wadau wengi wakiwemo madaktari kote nchini watakaowafanyia tathmini wafanyakazi waliopata madhara mahala pa kazi.

Sebera pia alitoa wito kwa wadau kutembelea banda la WCF ili kujipatia maelezo ya kina ,kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko huo ikiwemo Fidia kwa Wafanyaakzi ambayo inaanza kutolea Julai mosi mwaka huu wa 2016.Banda la WCF liko kwenye ukumbi wa Sabasaba kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere.
Waziri akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakzi wa WCF, na maafisa wa SSRA.

Waziri akiagana na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Fedha na Mipango, Ben Mwaipaja, baada ya kutembelea Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwenye Jengo la Wizarabya Fedha, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Julai 2, 2016. Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano cha SSRA, Sarah Kibonde Msika.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog