Jumapili ya November 29 klabu ya Arsenal itashuka dimbani kucheza mchezo wake wa Ligi Kuu Uingereza dhidi ya Norwich City katika uwanja wa Carrow Road, huu utakuwa mchezo wa 14 kwa Arsenal, Arsenal ambao watacheza mchezo wao November 29 mjini Norwich wamesafiri leo November 28 kuelekea huko ila safari yao imeingia katika headlines.
Arsenal ambao wameamua kusafiri kwa kutumia ndege binafsi kutoka London kwenda Norwich
wameingia katika mzozo na watu wa mazingira kutokana na kusafiri kwa
kutumia ndege ambayo imetumia dakika 14 hivyo wanadaiwa kuchafua
mazingira, kwani safari ya umbali mfupi wangeweza kutumia usafiri wa
basi.
Hata hivyo kocha wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger
amejitetea na kujibu kuwa wameamua kutumia usafiri wa ndege kutokana na
barabara kuwa katika matengenezo, hivyo kama wangetumia usafiri wa basi
wangekaa sana njiani, ndio maana wamefanya hivyo kukwepa msongamano.
Hii sio mara ya kwanza kwa Arsenal kuingia katika mzozo
na watu wa mazingira kwa kosa kama hilo, kwani waliwahi kuingia katika
headlines hiyo mwaka 2012 baada ya kusafiri umbali wa maili 100 kwa
kutumia ndege binafsi.
0 maoni:
Post a Comment