Saturday, November 28, 2015


Bado watu wengi wanaogopa jiji la Paris Ufaransa kutokana na hali ya kiusalama kuaminika kuwa ndogo, Paris iliingia katika headlines November 13 2015 baada ya kufanyika shambulio la kigaidi, tukio ambalo lilifanya baadhi ya wachezaji wa Paris Saint Germain kuogopa kurejea Paris kutokana na kuhofia usalama wa maisha yao.
Tukio la shambulio la kigaidi lilitokea November 13 siku ya mchezo wa kirafiki kati ya Ufaransa dhidi ya Ujerumani mchezo ulichezwa uwanja wa Stade de France na kusababisha baadhi ya wachezaji kulala uwanjani kutokana na hali ya usalama kwa baadhi ya mitaa ya Paris kutokuwa nzuri licha ya kuwa hawakushambulia uwanjani hapo, watu 130 walipoteza maisha kufuatia shambulio hilo, klabu ya PSG ambayo makao makuu yake ni Paris imeamua kuimarisha usalama wa wachezaji wake.
psg-favorit-marseille-monaco-pengusik-700x500
Awali Edson Cavani na David Luiz walikuwa wanaogopa kurudi Paris ila klabu yao imeamua kuwaongezea ulinzi wachezaji wote katika makazi yao binafsi . Winga wa kimataifa wa Brazil Lucas Moura amethibitisha kuwa uongozi wa klabu yao kuweka ulinzi katika makazi ya mastaa hao pamoja na kubadili utaratibu wao wanapokwenda uwanjani.
187122915_3037682
Lucas Moura
“Wameongeza ulinzi majumbani kwetu, klabu imeweka ulinzi katika milango ya nyumba za wachezaji, lakini pia tuna utaratibu mwingine wakati tunapokuwa tunaenda uwanjani hatutembei tena mbele ya mashabiki kama ilivyokuwa awali ila tunaenda na basi moja kwa moja hadi katika Parking za magari” >>> Lucas Moura

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog