Mpaka dakika 90 zinamalizika Malawi 1-0Tanzania (Agg:1-2)
Ushindi wa Nyumbani wawabeba Taifa stars leo Ugenini kwenye Uwanja wa Kamuzu Stadium, Blantyre - Malawi.
Tanzania wamefanikiwa sasa kuvuka na wanasonga mbele kwenye Raundi ya Pili watakwaana na Algeria ambao wanaanzia hatua hii ya raundi ya pili.
Washindi wa Raundi ya Pili wataingizwa kwenye Droo ya kupanga Makundi 5 ya Timu 4 kila mmoja ambapo Washindi wake wataenda Fainali Russia moja kwa moja.
Katika Mechi ya Kwanza iliyochezwa Jumatano iliyopita Tanzania iliichapa Malawi 2-0 kwa Bao za Maprofeshanali Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu ambao wote hucheza huko Congo DR kwenye Klabu ya Lubumbashi TP Mazembe.
Leo, Wamalawi walicharuka na kutawala, hasa Kiungo, dhidi ya Kikosi cha Tanzania chini ya Kocha Charles Boniface Mkwasa na kupata Bao lao la pekee la Mechi hii katika Dakika ya 41 kupitia kwa Banda.
Tanzania sasa watacheza Raundi ya Pili na Algeria ambao wanaanzia hatua hiyo ambayo Mechi zake zimepangwa kuchezwa Jijini Dar es Salaam Novemba 9 na Marudiano huko Algiers hapo Novemba 17.
Washindi wa Raundi ya Pili wataingizwa kwenye Droo ya kupanga Makundi 5 ya Timu 4 kila mmoja ambapo Washindi wake wataenda Fainali Russia moja kwa moja.
KOMBE LA DUNIA 2018
MATOKEO
Afrika-Raundi ya Awali- Marudiano
Jumapili Oktoba 11
Malawi 1 v 0 Tanzania - Agg:[1-2]Tanzania win
Ethiopia 3 v 0 Sao Tome And Principe - Agg [3-1]
Kenya 0 v 0 Mauritius [5-2]
0 maoni:
Post a Comment