Friday, October 2, 2015

Kuchagua chuo sometimes inakuwa kazi ngumu sana kwasababu unajikuta na maswali mengi sana baadhi yakiwa; je campus unayoitaka ina mazingira mazuri ya kusomea, usafiri wa kufika chuoni unapatikana, huduma za maduka je zipo? lakini swali kubwa kuliko lote ni, je maisha ya mwanafunzi wa kawaida chuoni hapo yakoje!?
IGIG
Sasa kwa mujibu wa mtandao wa Time wa Marekani, wanafunzi waliomaliza High School yani A-level sasa hivi wameamua kutumia Instagram kuchagua vyuo vya kujiunga navyo! Yes Instagram mtu wangu, kwanini?
IGIG7
Kutokana na majibu ya utafiti uliyofanyika, wanafunzi wengi wamelalamika kuwa wanapata shida kujua vitu vidogo vidogo kuhusu vyuo wanavyofikiria kujiunga navyo, haswa kujua hali halisi ya maisha ya wanafunzi wa kawaida vyuoni… Wengine wamesema vipeperushi’ vinavyotolewa na vyuo vingi havijibu maswali ya hali halisi ya maisha vyuoni na ndio maana wengi wameamua kutumia Instagram ili waweze kuchunguza wenyewe maisha ya kawaida ya kila siku vyuoni yakoje, kujua kama vyuo hivyo vitawafaa!
IGIG3
Utafiti uliofanyika umesema kuwa social network ya Instagram siku hizi ina nafasi kubwa sana ya kumshawishi mwanafunzi kujiunga au kutojiunga na chuo husika kutokana na picha zinazopostiwa kwenye account za wanafunzi wa vyuo mbalimbali, zikionyesha mazingira halisi ya campus hizo pamoja na uhalisia wa maisha ya kila siku kitu ambacho hakipatikani kwenye vipeperushi vya matangazo au kwenye websites za vyuo vingi.
IGIG4
>>> “mimi binafsi nilichunguza account nyingi za watu kwenye Instagram ili kuona tu maisha ya kawaida ya wanafunzi yakoje… ni kama kufanya tour ya chuo husika bila wewe kwenda chuoni hapo na kutembelea kila sehemu yani ofisini, madarasa, viwanja vya michezo na hata kupata picha ya maisha ya kila siku … vyote navifanya kwenye Instagram sasa hivi! <<< Morgan Levy mwanafunzi.
IGIG5
>>> “kuna chuo kimoja nilikifuatilia lakini nikagundua kuwa wanafunzi wengi wa pale wanapenda sana starehe na party nyingi kitu ambacho sikukifurahia sana…” <<< Morgan Levy.
Hii imekaa poa sana mtu wangu kwasababu ni rahisi na wala haina gharama yoyote ile, au wewe unaonaje? Kitu hiki kitawafaa wanafunzi wetu wa Tanzania!?

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog