Kocha
Mkuu wa timu ya Taifa Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya
Kilimanjaro Premium Lager, Charles Boniface Mkwasa leo ametangaza kikosi
cha wachezaji 28 watakoingia kambini Jumapili jioni kujiandaa na mchezo
dhidi ya Algeria Novemba 14 jijini Dar es salaam, na marudiano
kufanyika Novemba 17 nchini Algeria.
Akiongea
na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam,
Mkwasa amesema kikosi chake hicho kitaweka kambi nchini Omani kwa
takribani siku 10 kujiandaa na mchezo kuwania kufuzu kwa hatua ya
makundi ya Kombe la Dunia nchini Urusi mwaka 2018 dhidi ya Algeria.
Katika
kikosi hicho, Mkwasa amewaita wachezaji wapya sita wakiwemo Salim
Mbonde, Jonas Mkude, Salum Abubakar, Elias Maguri, Ramadhani Kessy na
Malimi Busungu na kufanya idadi ya wachezaji 28.
Wachezaji
aliowaita ni Magolikipa ni Ally Mustafa (Yanga), Aishi Manula (Azam),
Said Mohamed (Mtibwa Sugar), walinzi wa pembeni Kessy Ramadhani, Mohamed
Hussein (Simba), Juma Abdul, Haji Mwinyi (Yanga) na Shomari Kapombe
(Azam), Walinzi wa kati ni Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Hassan Isihaka
(Simba), Kelvin Yondani na nahodha Nadir Haroub (Yanga).
Viungo ni
Salum Telela (Yanga), Salum Abubakar, Himid Mao, Mudathir Yahya, Frank
Domayo (Azam), Jonas Mkude na Said Ndemla (Simba), washambuliaji wa
pembeni Farid Musa (Azam), Saimon Msuva (Yanga) na Mrisho Ngasa (Free
State Stars – Afrika Kusini).
Washambuliaji
wa kati ni John Bocco (Azam), Elias Maguri (Stand United), Ibrahim
Hajibu (Simba), Malimi Busungu (Yanga), Mbwana Samata na Thomas
Ulimwengu (TP Mazembe – Congo DR).(P.T)
0 maoni:
Post a Comment