Saturday, October 31, 2015



Chelsea wana kibarua tena wikendi hii watakapowakaribisha nyumbani Liverpool kwenye Ligi ya Premia Jumamosi.
Vijana wa Jose Mourinho wamekuwa wakiandikisha matokeo mabaya msimu huu, meneja huyo anakabilisha na shinikizo la kubadili mambo.
Chelsea wameshinda mechi moja pekee kati ya sita walizocheza karibuni zaidi katika mashindano yote.

The Blues wamefungwa mabao 19 Ligi ya Premia na ni Norwich (21), Bournemouth na Newcastle (wote wakiwa na 22) ambao wamefungwa mabao mengi zaidi msimu huu.
Ingawa huenda mshambuliaji wao Diego Costa akacheza, bado kuna shaka kumhusu Pedro ambaye anafuatiliwa kwa karibu baada yake kurejelea mazoezi.
Hata hivyo watakuwa bila Branislav Ivanovic na Thibaut Courtois. Nemanja Matic, aliyepigwa marufuku mechi moja atarejea uwanjani baada ya kutimikia marufuku hiyo mechi dhidi ya Stoke katika League Cup.
Upande wa Liverpool, meneja wao mpya Jurgen Klopp ataweza kumtumia Christian Benteke lakini Daniel Sturridge bado anauguza jeraha, Kolo Toure vilevile.
Akizungumza na wanahabari leo Mourinho amesema: “Matokeo sasa yamekuwa kila kitu (hasa kwenu wanahabari). Ni jambo la kushangaza kwamba miezi michache iliyopita nilishinda mechi nyingi na nikawa bingwa wa Uingereza, watu walikuwa wakisema kuna mambo muhimu zaidi kushinda matokeo.”
Kwa upande wake, Klopp amesema Chelsea bado ni hatari.
“Sina uhakika kwamba ni rahisi kucheza dhidi ya Chelsea leo kuliko mwaka jana. Mbona iwe hivyo?”

Liverpool walishinda mechi tatu mfululizo Stamford Bridge mwaka 2011 lakini hawajashinda hata mechi moja tangu wakati huo.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog