Stori nyingi na matukio mengi tumewahi
kuyasikia na kuyaona yakitokea uwanjani kama wachezaji kuvunjana miguu,
kuanguka na kupoteza fahamu wakati mwingine hata kupoteza
maisha uwanjani. Matukio yote hayo tumekuwa tukiyaona yakimalizika
uwanjani au adhabu hutolewa na Shirikisho au kamati husika, basi hii ni
tofauti kidogo kwa Uingereza mchezaji amefungwa jela kwa kosa la kumvunja mguu mchezaji wa timu pinzani wakati wa mchezo.
Mchezaji wa Sunday Ligi nchini Uingereza Nathaniel James Kerr amehukumiwa kifungo cha miezi 12 jela baada ya kukutwa na hatia ya kumvunja mguu mchezaji wa timu pinzani. Nathaniel James Kerr ambaye ana umri wa miaka 27 amehukumiwa September 30 jijini Manchester katika mahakama ya Minshull.
Inaripotiwa kuwa Nathaniel James Kerr aliwahi kuingia katika malumbano na mchezaji aliyemvunja mguu August 31 2014 katika mechi za mwanzo za Sunday Ligi. Nathaniel James Kerr
alipelekwa mahakamani baada ya kuonekana akijivunia kumvunja mguu
mchezaji wa timu pinzani kwa makusudi. Hivyo kosa lake lilikuwa
linahusishwa na chuki wala sio kosa la bahati mbaya.
0 maoni:
Post a Comment