Thursday, September 10, 2015



Wakati viongozi wengi wa siasa na wale wa serikali wanaona michezo ni kama burudani tu, England imefanikiwa kuingiza mamilioni ya fedha kwa mwaka jana tu na kujiongeza kiuchumi kupitia soka.


Watalii wanaofikia 800,000 kutoka nje ya England wametembelea nchini hiyo kwenye viwanja mbalimbali vya mpira wa miguu na kuisaidia England kuingiza pauni milioni 684.

Fedha hizo zingeweza kuinua kwa kiasi kikubwa uchumi wa Tanzania kama ingezipata kupitia fedha.

Fedha hizo ni zaidi ya zile ambazo Tanzania huingiza kupitia utalii hapa nchini.

Uwanja unaomilikiwa na Manchester United wa Old Trafford wenyewe ndiyo umetembelewa zaidi sawa na ule wa Emirates wa Arsenal. Kila mmoja umetembelewa na watalii 109,000.

Pamoja na kuyumba katika ligi, lakini watalii 99,000 walitembelea Anfield wa Liverpool na Chelsea ikapanda kwa kupata watalii 89,000 kupitia Stamford Brigde.


Hii inaonyesha kiasi gani mchezo wa soka ukiendelezwa unavyoweza kugeuka na kuwa kitegauchumi kwa watu binafsi lakini hata serikali.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog