Saturday, May 30, 2015


Nahodha wa zamani wa England, Rio Ferdinand, ameamua kustaafu Soka.
Ferdinand, mwenye Miaka 36, alimpoteza Mkewe Rebecca aliezaa nae Watoto Watatu hapo Mei Mosi Mwaka huu baada kuugua kansa na kufariki.
Katika maisha yake ya Soka aliichezea Timu ya Taifa ya England mara 81 na pia kuwa Nahodha wake.
Kwenye Klabu, Ferdinand alizichezea West Ham, Leeds United, Man United na kumalizia Msimu huu akiwa QPR ambayo imeshushwa Daraja toka Ligi Kuu England.
Akiwa na Man United, Ferdinand alitwaa Ubingwa wa England mara kadhaa na pia UEFA CHAMPIONS LIGI pamoja na Klabu Bingwa ya Dunia.
Akitangaza kustaafu, Ferdinand alitoa shukran kwa Mameneja na Wafanyakazi wa Klabu alizopitia pamoja na Familia yake na hasa Mkewe.
Ferdinand akisherekea Ubingwa akiwa na Klabu ya  Manchester United mwaka  2003 Kwenye Ubingwa wa Ligi Kuu England akiwa na  David Beckham kwenye picha.

Ferdinand akipeana mkono  na Kaka yake  Anton walipokutana Uso kwa uso na  Manchester United dhidi ya West Ham huko Upton Park mnamo mwaka 2005.

Ferdinand akishangilia na  Wes Brown  2006. Man United walipoitwanga  Wigan bao 4-0

Siyo tu kwenye Ushindi Rio Ferdinand pia alipokuwa akiukosa ushindi Aliumia na hapa walitolewa nje England kwenye Kombe la Dunia

Cristiano Ronaldo mwezi wa tano mwaka  2007 huko  Old Trafford walipoutwaa ubingwa na hapa Ferdinand alipata picha ya pamoja.

Ferdinand akiwa na  Joe Cole mwaka 2008 hukoM oscow

Nemanja Vidic, Anderson, Patrice Evra, Edwin van der Sar, Carlos Tevez, Ferdinand, Brown, Ryan Giggs na Mikael Silvestre wakishangilia baada ya kuitwanga Chelsea huko Moscow mnamo mwaka 2008

Ferdinand akipozi na  Ferguson pamoja na  Giggs na kombe lao mwaka 2008
2009
Manchester United kwenye picha ya pamoja mwaka  2009 walipoibuka na Ubingwa.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog