Van Gaal-Kocha wa Man UnitedMeneja
wa Chelsea Jose Mourinho amesema Manchester United ni tishio licha ya
kukabiliwa na Majeruhi kadhaa kitu ambacho Meneja wa Man United Louis
van Gaal amesema kitatoa nafasi kwa Wachezaji wengine.
Hii itakuwa mara ya pili kwa Jose Mourinho na Louis van Gaal, ambao walikuwa pamoja huko Barcelona Miaka 20 iliyopita wakati Van Gaal akiwa Meneja na kumpa nafasi Mourinho kuwa Msaidizi wake, kukutana Nchini England baada ya kutoka Sare 1-1 Old Trafford Mwezi Oktoba.
Mourinho, ambae Timu yake Chelsea ipo Pointi 8 mbele ya Timu ya 3 Man United na pia wana Mechi 1 mkononi, amesema: "Kikosi chao kinashangaza. Kila Wiki naangalia Vikosi vya Wapinzani na Wiki hii nilishangazwa na Wachezaji waliokuwa nao."
Mourinho, akiongea na Wanahabari, aliongeza: "Mnataka nitaje Wachezaji wao? Mata, Di Maria, Januzaj, Rooney, Van Persie, Herrera, Carrick, Blind, Fellaini...Mabeki? Rafael na Valencia, Luke Shaw Beki wa Kushoto, Sentahafu Smalling.....ndio watawakosa Evans na Jones, lakini wapo Blackett, McNair. Washacheza hawa. Van Gaal ni Kocha bora kuendeleza Vijana!"
Mourinho atamkosa Straika wake mkubwa Diego Costa ambae anasumbuliwa na Musuli za Pajani.
Nae Van Gaal, akiongea na Wanahabari, amekiri kukosekana kwa Wachezaji wake Majeruhi, hasa Blind na Carrick, kunaweza kumfanya amrudishe Kepteni Wayne Rooney kucheza kama Kiungo Mkabaji na hii itafungua njia kwa Robin van Persie kuanza kama Straika baada ya kuwa nje kwa Miezi Miwili akiuguza Enka yake.
Lakini habari njema kwa Van Gaal ni kupona kwa Fulbeki wa Kushoto Luke Shaw ambae alikuwa Majeruhi kwa Wiki 6.
Akizungumzia mbio za Ubingwa, Van Gaal amesema ingawa upo uwezekano kwao kutwaa Ubingwa lakini hali halisi ni kuwa Chelsea ndio wana nafasi kubwa kushinda.
Hata hivyo, Van Gaal amesisitiza kuwa wao hawakati tamaa na wataipa presha Chelsea hadi mwisho.
Kwenye Mechi hii muhimu ya Ligi Kuu England itakayochezwa Stamford Bridge Jumamosi, Man United itawakosa Wachezaji muhimu Wanne ambao ni Michael Carrick, Marcos Rojo, Daley Blind na Phil Jones.
Lakini Mourinho amesisitiza Kikosi cha Louis van Gaal, ambacho kimeshinda Mechi zao 6 zilizopita, kina Wachezaji wengi na ni rahisi kuziba mapengo.

0 maoni:
Post a Comment