Tuesday, April 14, 2015

Simba
Klabu ya Wekundu wa Msimbazi Simba SC, imepigwa faini ya sh. 300,000 na TFF kupitia kamati yake ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi Kuu mara baada ya timu yao kugoma kuingia kwenye vyumba vya kuvalia nguo (changing room) kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga wakati wa mechi dhidi ya Kagera Sugar.  Hatua hiyo ilisababisha wachezaji wakaguliwe kwenye gari lao. Katika mchezo huo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1.  Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa kanuni ya 14(9) ya Ligi.
Katika hatua nyingine pia Simba imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kuzingatia kanuni ya 14(13) ya Ligi Kuu baada ya vilevile kugoma kuingia vyumbani wakati wa mapumziko kwenye mechi hiyo hiyo namba 146 iliyochezwa Aprili 6, 2015.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog