|
Kutoka
kushoto ni Juma Herman(meneja wa Green Palm Hotel, Issaya Mwakilasa aka
Wakuvwanga, Jhikolabwino Manyika, Kelvina John, Mwenyekiti Masoud
Kipanya na Tonny Alphonce(Mtangazaji Metro fm 99.4 |
Siku ya Ijumaa ya tarehe 17/04/2015 ujumbe wa Imetosha Foundation
ukiongozwa na Mwenyekiti Masoud Kipanya ulifanya mahojiano katika kituo
cha redio cha Metro Fm 99.4 kwenye kipindi cha Pambazuko la Metro fm
99.4 ikiwa ni katika mfululizo wa kujitambulisha kanda ya ziwa kwa
taasisi hiyo inayopinga mauaji kwa watu wenye ualbino kwa njia ya
elimu.
Msanii
wa vichekesho (comedian) Wakuvwanga ambaye ni mjumbe wa taasisi hiyo
alitoa kali alipoulizwa angependekeza adhabu gani kwa watakaopatikana na
hatia ya kuua watu wenye ualbino? akajibu "Kwa kuwa hawa si watu bali
ni wanyama kutokana na vitendo vyao viovu basi napendekeza serikali
iwapeleke Mikumi national park iwafungie ndani ya senyenge ili watalii
wawe wanaenda kuwaona kama wanavyoenda kuwaona Simba na wanyama wengine!
Kipindi hicho maridhawa kiliendeshwa na watangazaji Tonny Alphonce na
Katumba Madua
|
Mtangazaji wa kipindi cha Pambazuko la Metro Fm, Tonny Alphonce akimuuliza swali Masoud Kipanya. |
|
Masoud Kipanya akijibu swali toka kwa mtangazaji wa Metro Fm 99.4zaji Tonny Alphonce. |
|
Tonny akimpiga swali Wakuvwanga, anayesikiliza kwa umakini wa hali ya juu, soma uone jibu lake! |
|
Kutoka kushoto ni Katumba Madua, Wakuvwanga na msanii wa muziki wa Reggae Jhikoman |
|
Moja ya studio za Metro Fm 99.4 ambazo wanazo tatu katika jengo hilo lililopo kati kati ya jiji la Mwanza |
|
Picha
ya Pamoja ndani ya Metro fm 99.4 toka kushoto ni Juma Herman, Mkala
Fundikira, Kelvina John, George Binagi, Tonny Alphonce, Rosier, Sophia
George, Wakuvwanga Masoud na Katumba Madua. |
|
Jhikoman kushoto, Rosier(receiptionist) na Masoud. |
|
Masoud
akibadilishana mawazo na Sphia George wa Metro fm 99.4 ya Mwanza wiki
iliyopita ujumbe wa Imetosha Foundation ulipotembelea studio za kituo
hicho cha redio. |
0 maoni:
Post a Comment