
9:25 PM

Unknown
Ijumaa
Aprili 24 Mchana huko Nyon, Uswisi kwenye Makao Makuu yao, UEFA
itaendesha Droo maalum za kupanga Mechi za Nusu Fainali za Mashindano
yao makubwa kwa Klabu za Ulaya yale ya UEFA CHAMPIONS LIGI na EUROPA
LIGI.
Jana UEFA CHAMPIONS LIGI ilikamilisha Mechi zao za Marudiano za Robo Famili na Timu 4 zimetinga Nusu Fainali.
Timu
hizo 4 ni Mabingwa Watetezi Real Madrid na wenzao wa Spain, FC
Barcelona, Mabingwa wa Italy, Juventus na Mabingwa wa Germany, Bayern
Munich.
Droo hii ni huru ikimaanisha Timu yeyote inaweza kupangwa na
yeyote na hivyo upo uwezekano wa hata kupata El Clasico lile pambano
kabambe kati ya Real Madrid na Barcelona.
Mechi za Nusu Fainali zitachezwa Mei 5 na 6 na Marudiano ni Mei 12 na 13.
0 maoni:
Post a Comment