Timu ya Taifa ya soka
ya Tanzania katika michuano ya ufukweni leo imeshindwa kuutumia vizuri
uwanja wake wa nyumbani mara baada ya kukubali kichapo kikali cha goli
6-2.
Walikuwa ni Tanzania
ambao walianza mchezo katika morali nzuri ila mashambulizi yakiwa ya
kushtukiza katika fukwe hizo za Escape One walifanikiwa kupata bao la
kwanza kipindi cha kwanza na mfungaji akiwa ni Ally Rabbi.
Haikuchukua muda mrefu
sana mchezaji Mwalimu Akida aliwainua mashabiki waliokuwepo katika fukwe
hizo mara baada ya kujipatia timu hiyo goli la pili na kuwafanya
Tanzania waongoze kwa goli hizo 2.
Waarabu wa Misri
walirejea vizuri wakiwa kama wanacheza kwenye uwanja wao walimiliki
mpira kwa asilimia kubwa zaidi huku wakifanya mashambulizi makali zaidi
pia wakikosa magoli mengi.
Misri walifunga bao lao
la kwanza kipindi cha pili kupitia kwa mchezaji wao Islam Ahmed,
mapema baada ya kupata bao hilo waliendelea kujituma zaidi na hatimaye
kupata bao lingine lililofungwa na Yehia Ally ambaye alifunga goli 4
peke yake leo, Goli jingine lilifungwa na Mohammed likiwa ni goli la 4
huku msumali wa mwisho ulimaliziwa na Yehia Ally na kukamilisha idadi ya
mabao 6-2 kutoka kwa waarabu hao.
Tanzania sasa inabidi ijiandae kikamilifu kwenda kupambana na Mafarao hao wa Misri nchini kwao baada ya wiki moja.
0 maoni:
Post a Comment