
Cristiano Ronaldo na Lionel Messi kwenye nyasi za Uwanja wa Old Trafford leo kwenye Mchezo wa kirafiki.
Raphael Guerreiro ndie ameipa ushindi Portugal katika dakika za nyongeza
za kipindi cha pili kwenye dakika ya 90' +1. Bao lilitosha kuilaza
Argentina kwa bao 1-0.

Ilikuwa ni Messi V Ronaldo leo!

Kwenye
Uwanja wa Old Trafford palikuwa hapatoshi!! Kipindi cha kwanza
Argentina waliutawala mpira lakini kipindi cha pili Portugal walikuja na
mbinu na kuweza kuwabana na kupata bao dakika za majruhi kupitia kwa
Raphael Guerreiro.

Wote wawili ndio walikuwa Manahodha wa timu hizo, Messi akiongoza kikosi cha Argentina na Ronaldo Portugal.

Wakisalimiana mbele ya Waamuzi

Taswira!!! Ronaldo vs Messi nani kuibuka kinara!!? Old Trafford!

Kumbe Mnaongea!!!

Alama za kuongea pamoja hizi!!

Wawili hao walipiga stori za kutosha tu kabla ya mchezo wa kirafiki
kati ya Argentina na Ureno haujaanza kwenye Uwanja wa Old Trafford mjini
Manchester, England, leo.
Hata hivyo, walizungumza kwa staili ya aina yake kila mmoja akiziba mdomo wake.

0 maoni:
Post a Comment