
Vijana wa Skylight Band wakitoa burudani kwa mashabiki wao huku wakiongozwa na Mary Lucos (kushoto) katika show zao za kila Ijumaa kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar bila kusahau leo pia watakuwepo kuanzia saa tatu usiku.

Mashabiki wa Skylight Band wakiburudika na nyimbo mbalimbali zilizokuwa zikiporomoshwa na bendi hiyo.

Sony Masamba a.k.a Fally Ipupa wa Bongo akifanya yake jukwaani huku kushoto na kulia akisindikizwa na Aneth Kushaba AK47 na Mary Lucos

Pichani juu na chini ni washiriki wa shindano la Miss Ilala 2014 litakalofanyika Jumamosi hii ndani ya hoteli ya Hyatt Regency The Kilimanjaro wakitambulishwa mbele ya mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.

Washiriki wa shindano la Miss Ilala 2014 wakijimwaga uwanjani na burudani ya Skylight Band ndani kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar Ijumaa iliyopita.

Pichani
juu ni walimbwende wa shindano la Miss Ilala 2014 wakiwa kwenye picha
ya pamoja mara baada ya kutambulishwa rasmi kwa mashabiki wa Skylight
Band ambapo Jumamosi hii atapatikana mshindi wa taji hilo ndani ya
Hoteli ya Hyatt Regency The Kilimanjaro jijini Dar. 
Wanamanyoya wakiwakilisha vilivyo kwa ukodak.
RSS Feed
Twitter
11:28 PM
Unknown
0 maoni:
Post a Comment