
11:21 PM

Unknown
Mathieu Debuchy atakuwa nje ya Uwanja kwa Miezi Mitatu baada ya kufanyiwa operesheni ya Enka yake.
Debuchy,
mwenye Miaka 29, aliumia na kutolewa nje kwa Machela Arsenal
walipocheza na Manchester City na kutoka Sare 2-2 hapo Septemba 13.
Akithibitisha
habari hizi, Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema operesheni ya
Mchezaji huyo wa Kimataifa wa France ilienda vyema lakini kuwepo nje
kwake kwa muda mrefu ni pigo kubwa sana kwao.
Debuchy alinunuliwa
kutoka Newcastle mapema Julai mahsusi kumbadili Bacary Sagna aliehamia
Man City mwanzoni mwa Msimu huu baada ya Mkataba wake kumalizika na
mwenyewe kukataa kuongeza.
Wenger
amesema: “Tutajua baadae pigo hili ni kubwa kiasi gani tukishajua
tumembadilisha kivipi. Lakini ndio maana tulimnunua Calum Chambers!”
0 maoni:
Post a Comment