Wiki ijayo Suarez atasafiri kwenda Barcelona kupimwa Afya yake na kusaini Mkataba wa Miaka Mitano.
Hivi sasa Suarez yupo kwenye Kifungo cha Miezi Minne alichopewa na FIFA baada kumuuma Meno Beki wa Italy Giorgio Chiellini wakati wa Mechi ya Kombe la Dunia kati ya Uruguay na Italy huko Brazil hapo Juni 26.
Inaaminika Barcelona wameafiki kulipa Dau la Pauni Milioni 75 ambalo ndio lipo kwenye Kipengele cha Mkataba wa Suarez na Liverpool ikiwa atataka kuhama kabla Mkataba wake kumalizika.
Ikithibitisha kuhama kwa Suarez, taarifa ya Liverpool ilisema: “Liverpool FC inathibitisha Luis Suarez ataondoka Klabuni baada kufikia makubaliano ya Uhamisho na FC Barcelona. Mchezaji sasa yupo huru kukamilisha taratibu za Uhamisho.”
RSS Feed
Twitter
5:22 AM
Unknown
0 maoni:
Post a Comment