Nyota
anayewindwa: Msimu uliopita, Lukaku alifunga mabao 15 akiwa na klabu ya
Everton ambayo inakaribia kumsajili kwa mkataba wa kudumu. Romelu
Lukaku atakamilisha uhamisho wa kujiunga na Everton kwa dau la paundi
milioni 24 baada ya kutangaza kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii
wa Twita mchana wa leo akisema: Ni muda wa kuanza ukurasa mpya.
Inafahamika
kuwa nyota huyo mwenye miaka 21, ambaye msimu uliopita alikipiga
Goodison Park kwa mkopo atasaini mkataba wa miaka mitano na Everton na
kuvunja rekodi ya usajili ya klabu hiyo.Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa Ubelgiji aliyeiwakilisha nchi yake katika fainali
za mwaka huu za kombe la dunia nchini Brazil, amekuwa akihusishwa
kuondoka darajani majira yote ya kiangazi mwaka huu.Everton ameamua kumpa mkataba wa kudumu baada ya kuwa na rekodi nzuri ya kufunga mabao 15 msimu uliopita.Roberto
Martinez ameamua kuvunja rekodi ya dau la usajili la klabu ambapo dau
alilosajiliwa Marouane Fellaini la paundi milioni 15 lililokuwa
linashikilia rekodi.Nafasi
ya Lukaku katika klabu yake ya Chelsea ingefinywa zaidi na Diego Costa,
Fernando Torres na Didier Drogba aliyesajiliwa siku za karibuni.Hii
ni taarifa njema kwa mashabiki wa Eberton ambao jana walimshuhudia Ross
Barkley akijifunga mkataba wa miaka minne Goodison Park.
0 maoni:
Post a Comment