BAADA
kukirejesha Kikosi cha Netherlands kwao baada Fainali za Kombe la Dunia
toka huko Brazil, Kocha mpya Louis van Gaal Leo hii anatarajiwa kutua
Klabu yake Mpya Manchester United Jijini Manchester huku ikiwepo shauku
kubwa ya kuleta Wachezaji wapya.
Anga za Uhamisho huko Ulaya sasa zimejaa mategemeo makubwa kuwa kuanza kazi rasmi kwa Van Gaal huko Old Trafford kutashuhudia Mabingwa hao wa zamani wakiongeza Wachezaji wao wapya baada kuwaunua Anders Herrera kutoka Athletic Bilbao na Luke Shaw kutoka Southampton.
Wachezaji wapya wanaohusishwa sana Man United ni Kiungo wa Chile, Arturi Vidal, anaechezea Juventus ya Italy, Thomas Vermaelen, Nahodha wa Arsenal, na Wachezaji Watatu waliokuwepo kwenye Kikosi cha Netherlands huko Brazil chini ya Van Gaal, Daley Blind, Bruno Martins Indi na Stefan De Vrij.Ishu ya Vidal imeongezeka nguvu hasa baada ya Mchezaji huyo mwenyewe kukiri anaihusudu Man United na pia sababu ya Mchezaji wa Man United, Patrice Evra kwenda Juve, kitu ambacho kinaonekana kulainisha ujio wa Vidal huko Old Trafford.
Kuhusu Thomas Vermaelen, Nahodha huyo wa Arsenal anaaminika anataka kuihama Klabu yake kwa kukosa Namba na zipo taarifa ameshaafikiana maslahi binafsi na Man United na kinachochelewesha ni upande wa Arsenal ambao wanaitaka Man United waongeze Dau na pia Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, kutaka kupata mbadala wake kabla hajaruhusu aondoke.
Tetsi zaidi za Wachezaji hao wapya kwenda au kutokwenda Man United zitapatikana mara baada ya Louis van Gaal kutambulishwa rasmi huko Old Trafford hapo Alhamisi.
Ijumaa, Van Gaal na Kikosi chake cha Man United kitaruka kwenda California kupiga Kambi ya Mazoezi kabla ya kucheza Mechi yao ya Kwanza ya Ziara yao huko Marekani hapo Julai 23.

0 maoni:
Post a Comment