Wednesday, June 18, 2014


Ligi kuu England itaanza Agosti 16 na leo hii Ratiba ya Msimu mpya wa 2014/15 imetangazwa.
Mabingwa Manchester City wataanza Ugenini na Newcastle wakati Meneja mpya wa Manchester United, Louis van Gaal, atakuwa Nyumbani Old Trafford kucheza na Swansea City.
Arsenal wataanza Nyumbani kucheza na Crystal Palace na Chelsea wako Ugenini kuivaa Timu mpya iliyopanda Daraja Burnley.
Siku hiyo ya Ufunguzi, Anfield itashuhudia Timu yao Liverpool ikicheza na Southampton.
Bila shaka pambano la mwanzo la mvuto mkubwa ni lile litakalochezwa Etihad Agosti 23 kati ya Man City na Liverpool waliomaliza Nafasi ya Pili Msimu uliopita.
Hapo Agosti 9, Uwanjani Wembley, kutakuwa na pambano la Kufungua Pazia Msimu kugombea Ngao ya Jamii kati ya Man City, ambao ni Mabingwa, na Arsenal, Mabingwa wa FA CUP.
Man United na Meneja wao mpya kutoka Holland,  Louis van Gaal kuiongoza  Manchester United wakiwa Nyumbani Old Trafford.

Mabinwa Manchester City wana kazi nzito kuanzia Ugenini na Newcastle

Joe Hart akishangilia na wenzake msimu uliomalizika

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog