Thursday, June 19, 2014

Itakuwa Mechi ya ‘Kufa na Kupona’ maana yeyote atakaefungwa atakuwa na nafasi finyu mno kutinga Raundi ya Pili ya Fainali za Kombe la Dunia baada ya zote, England na Uruguay, kufungwa Mechi zao za Kwanza za Kundi D.
England walichapwa 2-1 na Italy na Uruguay kudundwa 3-1 na Costa Rica.
England warm up during an England training session ahead of the 2014 FIFA World Cup Brazil match against Uruguay at Arena de Sao PauloWachezaji wa England wakijifua Sao Paulo masaa 24 kabla ya kukutana uso kwa uso na UruguayMeneja wa England HodgsonEngland pose for a team photo Straika wa Uruguay Luis Suarez yuko fiti baada ya kupona maumivu ya Goti lakini watamkosa Nahodha wao Diego Lugano ambae ameumia Gotu na pia Maxi Pereira mwenye Kadi Nyekundu.
Mchezaji pekee wa England mwenye hatihati kucheza ni Alex Oxlade-Chamberlain ambae aliumia Goti lakini amerejea tena Mazoezini.
Hii ni Mechi ambayo England na Uruguay lazima zishinde.
Akiongelea Mechi hii, Luis Suarez, ambae ndie alietwaa Tuzo za Mchezaji Bora huko England, amesema: “Nawajua Wachezaji wote wa England. Ama ni wenzangu Klabuni au ni Wapinzani kwenye Mechi. 

Wana kasoro kwenye Difensi ambazo tunaweza kuzitumia.”
Lakini Straika wa England, Daniel Sturridge, anaecheza Klabu ya Liverpool pamoja na Suarez, amechochea moto kwa kutamka: “Nitafanya kila niwezalo tushinde mradi iwe ndani ya Sheria lakini sitajiangusha na wala sitashika Mpira Golini kwa sababu si hulka yangu!”
Maneno hayo moja kwa moja yamemlenga Suarez kwa matukio yake Siku za nyuma.



Uso kwa Uso
-Kwenye Fainali za Kombe la Dunia, England na Uruguay zimekutana mara mbili kwa Uruguay kushinda 4-2 Mwaka 1954 na kutoka 0-0 Mwaka 1966.
-Mara ya mwisho kukutana ni Machi 2006 Uwanjani Anfield kwenye Mechi ya Kirafiki na England kushinda 2-1 kwa Bao za Peter Crouch na Joe Cole.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog