Wednesday, June 4, 2014


Rais Roussef ametetea vikali maandalizi ya kombe la dunia Brazil
Rais wa Brazil Dilma Rousseff ametetea jinsi ambavyo taifa lake limetayarisha Kombe la Dunia litakaloanza juma lijalo jijini Sao Paulo.
Alisema kuwa michezo hiyo itakuwa yenye ufanisi mkubwa ijapokuwa kumekuwepo na kukosolewa kwa kuchelewa kwa nyanja na miundombinu mbalimbali.
Aliwaambia wanahabari kuwa matatizo ya aina ile ni ya kawaida kila mahali.
Bi Rousseff ambaye huenda akakumbwa na maandamano mapya ya kupinga serikali, alisema kuwa hawataruhusiwa kuvuruga mashindano hayo.
'Gharama ya demokrasia'
Maandamano ya kupinga gharama ya kuandaa michuano ya kombe la dunia Brazil

''Kila mahali duniani, miradi mikubwa ya uhandisi mara kwa mara hutatizika,” bi Rousseff aliwaambia wanahabari kutoka katika mataifa ya kigeni katika makazi ya rais jijini Brasilia.
Alisema kuwa hakuna anayeweza kutengeneza reli za chini ya ardhi isipokuwa labda Uchina.
Hayo aliyasema kuhusu kuchelewa kwa miradi ya miundombinu, jambo ambalo limewakera wananchi wengi wa Brazil waliotarajia kunufaika kutokana na kuboreswa kwa miundombinu hiyo.
Mifumo ya usafiri katika miji ya Cuiaba, Salvador, Recife na miji mingine mingi haijakamilishwa kwa kuwa juhudi zote zilielekezwa katika kukamilika kwa nyanja za kandanda zitakazotumika katika mashindano hayo.
Rais huyo alitaja kuchelewa huko kama ''gharama ya demokrasia yetu.''
Akizungumzia maandamano ya kupinga Kombe la Dunia la hivi majuzi- ambayo baadhi yaligeuka kuwa vurugu- rais alisema kuwa ingawa maandamano yaliambatana na demokrasia, maelfu ya polisi na askari zaidi watatumiwa kuhakikisha kuwa haitavuruga Kombe la Dunia.
''Tunawahakikishia watu wote usalama,” alisema.
'Uangalifu wa karibu'
Uwanja wa Sao Paulo

Zaidi ya watu milioni moja waliingia mitaani wakati wa michezo ya Confederation kuandamana kupinga ufisadi na kile wanachodhani ni matumizi ya kupindukia katika kutayarisha Kombe la Dunia.
Maandamano hayo ambayo mwanzo yalianza kama makusanyiko madogo ya watu waliopinga kuongezeka kwa naulikatika usafiri wa umma ulianza kuwa baada ya polisi kutumia mbinu nzito kuwatawanya waandamanaji.
Bi Rousseff alisema kuwa vikosi vya usalama vitafanya kazi kwa uangalifu wakati huu.
Kikundi kidogo chenye waandamanaji wanaopinga serikali kililenga mechi ya kirafiki iliyokuwa ikichezwa baina ya Brazil na Panama katikati ya jiji la Goianiasiku ya Jumanne.
Waandamanaji hao waliokusanyika karibu na uwanja walikemea gharama kubwa ya michezo hiyo huku wakisema kuwa pesa nyingi ingetumiwa kugharamia huduma za umma ili kupunguza kukosekana kwa usawa.
Michezo hiyo itaanza tarehe 12 mwezi Juni huku wenyeji Brazil wakichuana na Croatia jijini Sao Paulo.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog