Kuelekea uchaguzi mdogo wa Jimbo la Chalinze mkoani Pwani
lililoachwa wazi baada ya mbunge wake SAID BWANAMDOGO kufariki hivi karibuni
Chama cha Mapinduzi kimefanya kura ya maoni ili kumpata mrithi wa Jimbo hilo
atakayechuana na wagombea kutoka vyama vingine.
Katika kura hiyo ya maoni wagombea watatu wamejitokeza
kuwania nafasi ya ubunge wa Jimbo la Chalinze kupitia chama cha CCM akiwemo
mbunge wa zamani wa Jimbo hilo RAMADHAN MANENO, mwenyekiti wa zamani wa Yanga IMANI
MADEGA na mdau mkubwa wa soka hapa nchini na mwanachama wa Yanga RIDHIWANI
KIKWETE.
Baada ya kura kupigwa RIDHIWANI KIKWETE ndiye amepata Baraka
za wanaCCM kuingia kwenye kinyang’anyiro cha Ubunge kwa kumpa kura 758 huku IMANI
MADEGA akishika nafasi ya pili kwa kupata kura 335 na RAMADHAN MANENO akishika
nafasi ya tatu kwa kupata kura 206.
0 maoni:
Post a Comment