WAKATI
wafanyabiashara wakiapa kuendelea na mgomo wao hadi siku ya jumatano
baada ya kukutana na mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter
Msigwa na mkuu wa mkoa wa Iringa pamoja na TRA ,jeshi la polisi mkoani
hapa limewataka wafanyabiashara wanaotaka kufungua maduka yao
kufungua bila kutishwa na mtu na kama wanataka kufikisha taarifa
polisi ili kupewa ulinzi wa jeshi hilo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa
Ramadhan Mungi ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na mtandao huu wa
www.francisgodwin.blogspot.com kuhusiana kuwepo kwa vitisho vya
kikundi cha vijana wanaojiita watoto wa mbwa mwitu ambao wanaongoza
wa wafanyabiashara mjini hapa.
Kamanda Mungi alisema kuwa ni ruksa
kwa mfanyabiashara yeyote kufungua biashara yake kwa uhuru na kama
kuna mtu atapita kumtisha anapaswa kupiga simu polisi ili kuchukua
hatua kwa watoa vitisho hao .
Kwani alisema ni uhuru wa
mfanyabiashara kufungua biashara yake ama kutofungua na kuwa mtu
mwingine asitumie nguvu kumlazizisha mwingine kufunga ama kufungua.
Kamanda Mungi alitangaza namba yake ya
simu kwa ajili ya wafanyabiashara kutoa taarifa pale wanapotishwa
kuwa ni 0754612948
Wakati jeshi la polisi mkoa wa
Iringa likitoa taarifa hiyo ya kuwataka wafanyabiashara kuwa huru
kufungua maduka yao baadhi ya wafanyabiashara eneo la Ipogolo,
Mlandege, Kihesa na katikati ya mitaa ya mji wa Iringa walionyesha
kususia mgomo huo na kuendelea na biashara kama kawaida.
Mbali ya wafanyabiashara hao kugomea
mgomo huo kwa madai kuwa kila mmoja anajua marejesho yake benk ya
maeneo mengine bado maeneo ya uhindini na Miyomboni kwa mara ya
kwanza usiku wa leo wafanyabiashara walioshindwa kufanya biashara
mchana walionekana kufungua maduka yao hadi saa 4 usiku tofauti na
siku nyingine ambapo maduka hufungwa saa 12 hadi saa moja usiku. |
0 maoni:
Post a Comment