Mkuu wa mkoa wa Iringa, Dr. Christina Ishengoma leo amezungumza na wafanya biashara wa manispaa ya Iringa katika ukumbi wa community centre uliopo eneo la Kitanzini katika manispaa ya Iringa, mada kuu ilikuwa inahusu mgomo wa wafanya biashara kupinga mashine mpya za kutoa risiti zilizotolewa na TRA ili zitumike katika biashara zao.
baadhi ya wafanya biashara walio hudhuria katika mkutano huo uliofanyika leo.
Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Iringa,Bw. Lucas Mwakabungu, akizungumza na wafanya biashara katika mkutano huo.
baadhi ya wafanya biashara waliotoa mawazo yao katika mkutano huo
Wafanya biashara hao walidai kuwa hawazitaki mashine hizo kwa sasa kwa sababu haziwapi faida; husan wale wafanya biashara wadogo wadogo ambao kipato chao ni kidogo kwa kuwa mashine hizo zina gharama kubwa na matengenezo yake yana gharama kubwa pia hakupewa taarifa za kutosha kuhusu mashine hizo bali walishtuliwa tu hivyo hawajaridhika na uamuzi huo wa serikali kupitia TRA.
Polisi wa kutuliza ghasia wakiondoka katika eneo hilo la mkutano.
Wafanya biashara hao bado walionekana kutokuwa na furaha baada ya kufungwa kwa kikao hicho lakini hali ilikuwa kushoto kulia kwani wapo wafanya biashara walioonekana wakifungua maduka yao wakati maduka mengine yalikuwa bado hayajafunguliwa.
.
0 maoni:
Post a Comment