Friday, January 31, 2014




Wajumbe wa upinzani katika mazungumzo ya amani nchini Syria mjini Geneva
Awamu ya kwanza ya mazungumzo ya amani ya Syria itakamilika hii leo mjini Geneva, bila ishara ya mafanikio lakini kuna 'matumaini' anasema mjumbe wa umoja wa mataifa Lakhdar Brahimi.
Serikali ya Syria na waakilishi wa upinzani bado wana misimamo mikali juu ya maswala muhimu.
Lakini mpatanishi wa Umoja wa Mataifa anayeongoza mazungumzo hayo anasema anatumai awamu ya pili ya mazungumzo hayo itakayofanyika baada ya siku kumi zijazo italeta mafanikio kiasi .
Siku kumi baada ya umoja wa mataifa kuanzisha juhudi ya kumaliza vita wenyewe kwa wenyewe nchini Syria wajumbe kutoka pande mbili katika mgogoro huo bado wako kwenye meza moja ya mazungumzo.
Nwenyekiti wa mazungumzo hayo, Lakhdar Brahimi, anazingatia hilo kuwa ufanisi wa aina yake, huku akielezea kuwa kulikuwa na baadhi ya nyakati za hasira, lakini pia nyakati za matumaini.
Kisha akaelezea jinsi wajumbe wa pande zote mbili walipokubaliana kubaki kimya kwa dakika moja kukumbuka nyoyo za wale waliofariki katika mapigano nchini Syria.
Mazungumzo yamekuwa magumu lakini yenye matumaini kati ya serikali na upinzani.
"Tulikuwa na nyakati za hasi hali kadhalika nyakati zenye matumaini. Upinzani ulipendekeza tuwe na kimya cha dakika moja kuwaenzi waliokufa nchini Syria, bila kuzingatia kambi wanayotoka na ujumbe wa serikali mara moja ulikubali na kisha tukabaki kimya kwa dakika moja,'' amesema bwana Brahimi.
Lakini hapajakuwa na mafanikio makubwa katika mazungumzo kuhusu maswala muhimu yanayoikabili Syria kama vile ugavi wa madarakani na kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingizwa katika maeneo yaliyozingirwa.
Hata mpangilio wa jinsi maswala haya yanapaswa kushughulikiwa umezua malumbano.
Bwana Brahimi ana matarajio kuwa likizo ya siku kumi kwa wajumbe kuanzia baada ya kikao cha mwisho leo Ijumaa, itatoa hewa safi kwa pande zote kuzingatia mbinu bora zaidi za kushugulikia maswala hayo na pia kuwapa fursa wafadhili wao-marekani na Urusi kutumia ushawishi wao.
Mawaziri wa mashauri ya kigeni, John Kerry wa Marekani na mwenzake wa Urusi Sergev Lavrov watakutana wikendi hii mjini Munich nchini Ujerumani.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog