Friday, January 31, 2014

  

Marehemu Masoud Mohamed MC D enzi za uhai wake.


Marehemu Masoud Mohamed maarufu kama MC D mpiga tumba wa Bendi ya Twanga Pepeta amezikwa leo Saa Saba katika Makaburi ya Njoro yaliyopo Moshi Mkoani Kilimanjaro. Katika Mazishi ya Mwanamuziki huyo wadau mbalimbali wa muziki wa Dansi waliungana pamoja kumsindikiza MC D katika safari yake ya Mwisho. Marehemu MC D alifariki Siku ya juma tatu saa nne usiku katika Hospitali ya KCMC dakika chache baada ya kufikishwa hapo kwa matibabu. Hata hivyo wanamuziki wa bendi mbalimbali walikua wakimlilia huku wakikiri ya kuwa hakuna mpiga Tumba mahiri kama yeye na Kifo chake kimeacha pengo kubwa katika muziki wa dansi.



Ndugu na Jamaa wakiwa wanasubiri mwili wa MC D uandaliwe na kuwekwa katika Jeneza Tayari kwa Maziko.

Mpiga Drums wa Twanga Pepeta mwenye miwani nyeusi anayefahamika kwa Jina la MKIBOSHOO akiwa nje ya Nyumba ya kina MC D tayari kwa kumsindikiza Mwanamuziki mwenzake.

Baadhi ya wanamuziki na wapenzi wa muziki wa Dansi wakiwa wamekaa kwa majonzi eneo la nje la Msikiti wa Rahma uliopo Moshi ambapo Mwili wa Marehemu ulikua ukisaliwa kwa mara ya mwisho.

Wanamuziki na mdau wa Muziki wa Dansi Bahati aliyeweka mkono mfukoni wakijadili jambo nje ya msikiti wa Rahma.
Safari ya kuupeleka mwili wa MC D makaburini

Umati wa watu ukiusindikiza Mwili wa Marehemu MC D kuelekea Makaburini

Safari ya kuelekea Makaburi ya Njoro mahali atakapolazwa MC D

 Hii ndiyo nyumba ya Mwisho atakapolazwa MC D


Mwili wa Marehemu MC D ukitolewa katika Jeneza tayari kwa kuzikwa.

Mwili wa MC D ukihifadhiwa kaburini kwa Taratibu za Kiislam

Mdau wa Muziki wa Dansi Tanzania Ndugu Patrick Kisaka maarufu kama Dozee akishuhudia Mwili wa MC D ukihifadhiwa Kaburini.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog