-WAGOMBEA KOCHA BORA: SIR ALEX FERGUSON, JUPP HEYNCKES & JURGEN KLOPP!!
-WAGOMBEA KINAMAMA: MARTA, ABBY WAMBACH & NADINE ANGERER!
-MANDELA, EUSEBIO KUPEWA HESHIMA MAALUM KWENYE HAFLA!!
-WAGOMBEA KOCHA BORA: SIR ALEX FERGUSON, JUPP HEYNCKES & JURGEN KLOPP!! -WAGOMBEA KINAMAMA: MARTA, ABBY WAMBACH & NADINE ANGERER!
-MANDELA, EUSEBIO KUPEWA HESHIMA MAALUM KWENYE HAFLA!!
Wachezaji hao watatu walifuzu kuingia Fainali toka Listi ya Wagombea 23 na Mshindi kati yao atatangazwa kesho Januari 13 katika Hafla maalum.
Washindi wa Tuzo hizi hupatikana kutokana na Kura za Makocha na Manahodha wa Timu za Taifa Wanachama wa FIFA pamoja na Wawakilishi wa Wanahabari toka Dunia nzima wanaoteuliwa na Jarida la Soka la Ufaransa France Football.
Kwa upande wa Kinamama, Wagombea wa Tuzo ya Mchezaji Bora ni Nadine Angerer (Germany), Marta (Brazil) na Abby Wambach (USA).
Kocha
Bora atachaguliwa kutoka Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex
Ferguson, Kocha wa zamani wa Munich Jupp Heynckes na yule wa Borussia
Dortmund, Jurgen Klopp.
France Football ndio walioanzisha Ballon
d'Or Mwaka 1956 ili kumpata Mchezaji Bora Ulaya na Staa wa England,
Stanley Matthews, ndie alikuwa Mshindi wa Kwanza.
Mwaka 2007, Ballon d'Or iligeuka kuwa
Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani na kuanzia Mwaka 2010 ikawa FIFA Ballon
d'Or na Mshindi wake ni Messi tangu wakati huo.
Safai hii, baada ya kuitwaa Ballon d'Or
Mwaka 2008 akiwa na Manchester United, Cristiano Ronaldo, ndie
anaetegemewa kumpiku Messi ambae ameitwaa mara 4 mfulizo hadi 2012.
Wakati Ribery akitegemea mafanikio yake
na Klabu yake Bayern Munich yatamfanya afuzu, Ronaldo anategemea sana
Rekodi yake binafsi ya kupiga Bao nyingi ndio itampa Tuzo hiyo.
Na
hilo linampa nguvu Ronaldo kwani Tuzo hii ni ya Mchezaji binafsi na si
Timu na Goli zake 66 katika Mechi 56 kwa Klabu yake na Nchi yake kwa
Mwaka 2013 ndivyo vitakavyompa nguvu Ronaldo kutamba.
0 maoni:
Post a Comment