Kiongozi wa kanisa Katoliki
duniani Papa Francis amesema kuwa Internet ni zawadi kwa dunia nzima
kutoka kwa Mungu lakini akaonya kuwa matamanio ya kutaka kuwasiliana
zaidi kutumia Internet kunawatenga watu kutoka kwa familia na marafiki
zao.
Amewataka waumuni wa kikatoliki kujiunga na
mfumo wa dijitali. "Internet... inatoa nafasi ya mafanikio mengi. Hiki
ni kitu kizuri bila shaka ni zawadi kutoka kwa Mungu,'' alisema Papa.Papa mwenyewe ana akaunti kwenye Twitter ambayo ina wafuasi zaidi ya milioni kumi.
Amehimiza kuwa mawasiliano yanapaswa kuhusisha hisia na mawazo, watu kukutana na kujuliana hali.
Kadhalika amewataka waumini wa kikatoliki kutodhani kuwa ni mawazo yao na imani zao pekee ambazo ni muhimu wakati wakiwasiliana na watu wa dini nyinginezo.
0 maoni:
Post a Comment