Mchezaji mkongwe wa AC MILAN na timu ya
taifa ya uholanzi, Clarence Seedorf, Amekuwa Meneja mpya wa AC Milan ya
Italy baada kutangaza kustaafu kucheza Soka.
Clarence Seedorf:
-Umri: Miaka 37
-Uraia: Netherlands
-Klabu: Ajax (1992-95); Sampdoria (1995-96); Real Madrid (1996-2000); Inter Milan (2000-02); AC Milan (2002-2012); Botafogo (2012-2014)
-Holland: Mechi 87
Clarence Seedorf akiwa na kocha wa zamani wa Botafogo, Eduardo Hungaro
na amemtakia mafanikio mema ya mwaka 2014 huko Milan baada ya Milan
kumlima shoka kocha wake.
Clarence Seedorf akiwaaga wenzie wabrazil katika club ya Botafogo huko Rio de Janeiro-Brazil.
Jumapili iliyopita, AC Milan ilichapwa Bao 4-3 na Sassuolo.
Akiwa na AC Milan, Seedorf alicheza Mechi zaidi ya 400 na kutwaa Ubingwa wa Serie A mara 2 na UEFA CHAMPIONS LIGI mara 2.
Pia, Seedorf alikuwa Mchezaji wa Kwanza kutwaa UEFA CHAMPIONS LIGI mara 3 na Klabu 3 tofauti baada kushinda akiwa na Ajax Mwaka 1995, Real Madrid 1998 na AC Milan, Miaka ya 2003 na 2007.
Seedorf, ambae pia alizichezea Klabu za Inter Milan na Sampdoria, baada kuondoka AC Milan alijiunga na Klabu ya Brazil, Botafogo, Mwaka 2012.
0 maoni:
Post a Comment