Thursday, October 10, 2013

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali pingamizi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), na kuzikubalia kampuni tano za simu nchini kujiunga katika kesi ya kupinga tozo ya kodi za simu ya Sh 1,000 kwa kila laini kwa mwezi. 
SOMA ZAIDI.......
Kampuni hizo zinaungana na Chama cha Kutetea Walaji kupinga utekelezaji wa kodi hizo uliotakiwa kuanza Julai mwaka huu, baada ya kupitishwa bungeni Juni mwaka huu.

Akitoa uamuzi wa jopo, Mwenyekiti wa Jopo la majaji, Jaji Aloysius Mujuluzi, alisema wamekubaliana na hoja zilizowasilishwa na wakili wa kampuni tano za simu, Fatuma Karume, kwamba hati ya kiapo iliyowasilishwa mahakamani na wateja wake iko sahihi.

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali akimwakilisha AG aliwasilisha pingamizi la awali kupinga maombi ya kampuni za simu kujiunga katika kesi akidai kwamba, hati ya kiapo ilikosewa kisheria kwani aliyeapa ni mmoja, Tumaini Shija wa Kampuni ya TTCL.

“Tunakubaliana na hoja za Karume kwamba hoja za kupinga maombi ya kampuni za simu kujiunga katika kesi hayana msingi, kwa sababu sheria ina ruhusu mtu kuapa kwa niaba ya wengine.

“Kampuni tano za simu, MIC Tanzania Limited, Vodacom, Airtel, ZANTEL na TTCL zimekubaliwa kuingia katika kesi, watakuwa mlalamikaji namba mbili mpaka sita, mlalamikaji namba moja ni Chama cha Kutetea Walaji,” alisema Jaji Mujuluzi.

Jaji Mujuluzi alisema walalamikaji hao baada ya kuungana watafanya marekebisho ya hati ya maombi yao, na Oktoba 15 mwaka huu wataiwasilisha mahakamani, Jamhuri itawasilisha majibu, kisha Oktoba 21 maombi ya kupinga tozo za simu yatasikilizwa.

Mdaiwa katika kesi hiyo ni Wizara ya Fedha na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Chama cha Walaji kiliwasilisha maombi mahakamani dhidi Wizara ya Fedha hivi karibuni wakipinga tozo hiyo kwa madai kwamba inawaumiza wateja wao.

Wakili Karume akiziwakilisha kampuni za simu, aliwasilisha maombi mahakamani wakitaka waruhisiwe kujiunga katika kesi hiyo na wamekubaliwa.

Majaji wanaosikiliza kesi hiyo ni majaji watatu, Aloysius Mujuluzi (Mwenyekiti wa jopo), Jaji Laurence Kaduli na Jaji Salvatory Bongole.

Walalamikaji hao sita wamewasilisha maombi mahakamani hapo wakipinga sheria mbalimbali zinazokiuka Katiba.

 
Wanadai wateja wao hawana uwezo wa kulipa kodi ya Sh 1000 kwa kila laini ya simu iliyopitishwa bungeni Juni mwaka huu, hivyo wanaitaka Mahakama kuzuia

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog