Wednesday, October 9, 2013

Mbunge wa jimbo la bukoba mjini ambae pia ni waziri wa maliasili na utalii balozi khamisi kagasheki amelazimika kusitisha ziara ya kiserikali huko nchini Kuwait na kurudi jimboni kwake kwa ajili ya kuwafariji wananchi walioathilika na mafuriko.   Mara baada ya kuwasili alikutana na viongozi mbalilmbali na alipewa taarifa ya kila kata ili aweze kupata hali halisi ya madhala yalijitokeza kwa kila kata,  baada ya kupata taarifa  alianza ziara ya kutembelea waanga wa mafuriko na kuona hali halisi,mh kagasheki alishuhudia majumba yakiwa yamebomoka na ualibifu mkubwa wa vifaa,lakini pia watu wengi walikuwa hawana mahala pa kuishi kutokana na nyumba zao kujaa maji, Balozi kagasheki ameweza kutoa msaada wa chakula kwa waanga wote,lakini pia kwa wale ambao nyumba zao zimebomoka kuta ameweza kutoa pesa ili waweze kurekebisha , mh kagasheki alisema wakati serikali ikifanya tathimini yeye kama mbunge swala hili limemgusa sana kwa hiyo ameona afanye awezalo kwa haraka wakati taratibu zingine zikifanywa.

VIONGOZI MBALIMBALI KUTOKA KWENYE KATA ZA MANISPAA YA BUKOBA
BALOZI KAGASHEKI AKIPOKEA TAARIFA YA MAAFA YA MAFURIKO JIMBONI KWAKE

KATIBU WA CCM BUKOBA MJINI JANATH MUSA KAYANDA AKIELEZA KWA UFUPI MAENEO YALIYOATHILIKA NA MAFURIKO

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog