Monday, October 21, 2013



Standard Media wametoa taarifa nyingine ambayo inazidi kulipa shambulio la Westgate nguvu ya kuendelea kumiliki vichwa vya habari baada ya kuripoti kwamba Magaidi waliofanya hilo shambulio Nairobi mwezi September walitumia helikopta ambayo inamilikiwa na mwanasiasa maarufu wa zamani nchini Kenya ambae taarifa hii haijamtaja.

Imefahamika, sita kati ya magaidi walitumia helikopta hiyo kutoka kwenye kambi ya wakimbizi ya Dadaab mpaka Nairobi kwa kuhofia kushtukiwa mapema na kukamatwa iwapo wangetumia usafiri wa ardhini.

Wapelelezi wamesema wanaamini kwenye helikopta hiyo, magaidi hawa walibeba baadhi ya silaha za kivita ambazo zilitumika kwenye shambulio hili ambalo liligharimu maisha ya zaidi ya watu 60 akiwemo ndugu wa Rais Uhuru Kenyatta.

Magaidi hawa wanaaminika kuingia kwenye kambi ya Dadaab wakitokea Somalia miezi sita iliyopita ambapo walijifanya Wakimbizi huku wakiendelea kupanga shambulio la September 21 ambapo baadae walichukua hiyo helikopta ambayo tayari Pilot wake alikamatwa na kuhojiwa na kisha baadae kuachiwa.

Hata hivyo imegundulika pia ndani ya jumba la Westgate ambalo ndani yake lina maduka na migahawa mbalimbali, kwenye floor ya kwanza kulikua na raia wa Uturuki ambae alikodi chumba cha duka zaidi ya mwaka mmoja uliopita na kuanza kukitumia kwa biashara ya kuuza simu miezi sita iliyopita na pia chumba hichohicho kutumika na magaidi kama sehemu ya kuhifadhia silaha.
Raia huyu wa Uturuki alisafiri kwenda nje ya Kenya siku moja kabla ya shambulio la Westgate na Polisi wanaendelea na msako ambao pia unalihusisha gari aina ya BMW ambalo lilimilikiwa na yeye na kutumika kubeba Magaidi hawa kwenye mizunguko mbalimbali ya Nairobi.

Kwa kumalizia post hii, kingine cha kukwambia ni kuhusu Mwanamke mmoja aliefahamika kwa jina la Wanjiru kutoka kijiji cha Kangari huko Nyeri kugundulika kwua mmoja wa Magaidi na mpaka sasa Watu wa usalama wanandelea kufatilia kama na yeye aliuwawa kwenye majibizano ya risasi kati ya magaidi na vikosi vya usalama.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog