Monday, July 6, 2015


Wachezaji wa Liverpool wakiwa mazoezini leo hiiDejan na Lickie Lambert wakipasha
Jordan Henderson
Liverpool back trainingNathaniel Clyne kazini leo Liverpool
Raheem SterlingJoe Gomez nae ndani mazoezini


Wayne RooneyWayne Rooney kwenye gari akiingia mazoezini CarringtonMemphis DepayDepayRobin Van PersieDaley BlindWayne RooneyMichael Carrick na kipa Anders LindegaardRobin Van Persie


BONDIA Floyd Mayweather amepokonywa mkanda wa WBO uzito wa Welter alioshinda dhidi ya Manny Pacquiao- na Anthony Mundine ameomba kuzichapa naye Septemba.
Mayweather alishindwa kulipa wakati Ijumaa dola za KImarekani 200,000 ambayo ni ada ya mkanda kwa WBO na Kamati imeamua kumvua taji hilo mbabe huyo mwenye umri wa miaka 38. Inamaanisha Timothy Bradley JR anatarajiwa kuvikwa mkanda huo baada ya kumshinda kwa utata Jessie Vargas mwezi uliopita.
Mayweather bado ana siku 14 za kukata rufaa, ingawa uamuzi hautarajiwi kubadilishwa.

Floyd Mayweather (kushoto) amevuliwa mkanda wa WBO alioupata kwa kumshinda Manny Pacquiao

"Kamati ya ubingwa wa dunia ya WBO imeona hakuna namna nyingine zaidi ya kuendelea kumtambua Floyd Mayweather Jr. kama bingwa wa WBO uzito wa Welter duniani na kumvua mkanda kwa kushindwa kutimiza raratibu za mapambano ya ubingwa wa dunia wa WBO," imesema WBO Jumatatu.
Mayweather bado ni bingwa wa uzito wa Welter ma Super Welter wa WBC na WBA, ingawa mabondia hawaruhusiwi kushikilia mataji ya uzito tofauti.
Mayweather anatarajiwa kurejea ulingoni kwa mara ya 49 ambalo linaweza kuwa pambano lake la mwisho Septemba na Mundine – mshindani mkuu wa WBC katika uzito wa Super-Welter amemuandikia barua ya wazi bondia huyo kuomba awe mpinzani wake afuataye. 
MSHAMBULIAJI Memphis Depay amejiunga na wachezaji wenzake wa Manchester United kwa mara yaa kwanza tangu asajiliwe kwa Pauni Milioni 25 kutoka PSV.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 alikuwa sura mpya pekee viwanja vya Carrington jana wakati kikosi cha Louis van Gaal kiliporejea mazoezini kabla ya ziara ya Amerika kujiandaa na msimu mpya.
Depay alipigwa picha akiwa amevalia jezi namba 26 ambayo atakuwa anitumia United na inatarajiwa mashabiki hawatajali hilo zaidi ya kile atakachokifanya uwanjani.
Memphis Depay (wa pili kulia), akiwa mazoezini na wachezaji wenzake Man United, Wayne Rooney (kushoto), Phil Jones (kulia) na Michael

Depay trained for the first time as a Manchester United player
Depay was among the first team for the squad's return to pre-season training


KLABU ya Barcelona imefikia maubaliano na Atletico Madrid juu ya kumsajili kiungo Arda Turan kwa Pauni Milioni 29. 
Winga huyo mwenye umri wa miaka 28 alizivutia pia Chelsea na Manchester United, lakini Barcelona imeshinda mbio za kuwania saini yake. 
Barcelona italipa Pauni Milioni 24 mbele na nyingine Pauni Milioni 5 zitalipwa baadaye kufuatia mwanasoka huyo wa kimataifa wa Uturuki kusaini Mkataba wa miaka mitano.

Barcelona imeposti picha hii ya 'kubumba' ya Arda Turan akiwa na jezi ya klabu hiyo baada ya kutangaza kumsajili

Turan jetted off to meet his agent Ahmet Bulut as Barcelona last week as clubs battled for his signature


Chelsea were interested in signing Turan but he will now move to Spanish champions Barcelona

KIUNGO James Milner ametambulishwa kama mchezaji wa Liverpool leo na kusema kiu yake ni kushinda mataji na Medali kibao akicheza dimba la kati Anfield.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa England amesema anataka kuendeleza desturi ya kuinua mataji kama ilivyokuwa Manchester City baada ya kupata nafasi ya kufanya kazi na kocha Brendan Rodgers.
Ingawa hakusema moja kwa moja kuhusu Steven Gerrard baada ya kukabidhiwa jezi namba 7, Milner alisema pengo lililoachwa na gwiji wa Liverpool halitasumbua.
James Milner ametambulishwa leo Liverpool na kusema anataka kushinda mataji na Medali Anfield
James Milner has taken the No 7 shirt at Liverpool 

Milner said he hopes to show his best form straight away in a Liverpool shirt when the season begins
Milner said the appeal of regular football in central midfield at Liverpool was too good an offer to turn down



MKONGWE Andrea Pirlo ameondoka rasmi Juventus kuhamia New York City, klabu zote zimethibitisha.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Italia amecheza kwa miaka minne Juve ikiwa Serie A, na sasa ataungana na kiungo mwenzake mkongwe wa England, Frank Lampard timu hiyo ya Ligi Kuu Marekani, maarufu kama Major League Soccer itakayoanza Julai 21.
Pirlo anayetarajiwa kusaini Mkataba wa miezi 18, ameiambia tovuti ya klabu hiyo: "Nimekuwa nikihitaji uzoefu huu kwa muda mrefu na sasa fursa hii imekuja nataka kuichukua,"amesema. 
Andrea Pirlo ameondoka rasmi Juventus kuhamia New York City na klabu hiyo ya MLS imeposti picha katika tovuti yake
Pirlo will link up in midfield with new team-mate Frank Lampard in Major League Soccer from July 21

 
 
 
Pirlo poses in his new kit
Pirlo was at Yankee Stadium to watch New York City lose in their derby against Red Bulls last week
The Italian World Cup winner (centre) has completed a deal to join the Major League Soccer franchise
 
 

waliotembelea blog