Thursday, June 18, 2015


Klabu ya Liverpool imekataa rasmi ombi la pili la Manchester City la kutaka kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Raheem Sterling.
Inaaminika kuwa ombi hilo jipya lilikuwa la kitita cha pauni milioni 35.5 ambacho kingeongezwa na kufika pauni milioni 40.
Sterling mwenye umri wa miaka 20 ambaye amehusishwa na Arsenal pamoja na Real Madrid ana thamani ya pauni milioni 50 kulingana na Liverpool.

Wiki iliopita Liverpool ilikataa kitita cha pauni milioni 25 kutoka kwa Manchester City.
Sterling alijiunga na Liverpool kutoka QPR mwaka 2010 na sasa yuko katika kandarasi hadi mwaka 2017, lakini amekataa ombi la malipo ya kitita cha pauni 100,000 kwa wiki.


Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, imewasili leo asubuhi Visiwani Zanzibar tayari kwa maandalizi ya mchezo wa siku ya jumamosi dhidi ya timu ya Uganda kuwania kufuzu kwa CHAN 2016.
Msafara wa Taifa Stars unajumuisha wachezaji 21 na benchi la ufundi 7 ambao wamefikia katika hoteli ya Nungwi Inn, mchezo dhid ya Uganda utachezwa katika uwanja wa Amani kisiwani Zanzibar jumamosi kuanzia majira ya saa 2 usiku.

Stars inakutana na Uganda katika mchezo huo wa awali wa kuwania kufuzu kwa fainali za mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Rwanda, kabla ya kurudiana wiki mbili baadae katika uwanja wa Namboole jijini Kampala.
Mara baada ya kurejea kutoka nchini Misri kikosi cha Stars kiliendelea na kambi katika hoteli ya Tansoma na kufanya mazoezi katika uwanja wa Karume kabla ya kuondoka leo asubuhi kuelekea visiwani Zanzibar.
Kocha mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij amewaongeza wachezaji watano ambao hawakua katika kikosi kilichocheza dhidi ya Misri, kufuatia wachezaji wa kimataifa wa Tanzania kutoruhusiwa kucheza mchezo huo wa CHAN wikiendi hii.


MSHAMBULIAJI wa timu ya Stand United,Abasarim Chidiebele akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga mara baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia timu ya Coastal Union,Picha na Mwandishi Wetu,Tanga

MSHAMBULIAJI wa timu ya Stand United, Abasarim Chidiebele, amesaini mkataba wa kuitumikia timu ya Coastal Union kwa mkataba wa mwaka mmoja katika msimu ujao wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Chidiebele alitua mkoani Tanga juzi kwa ajili ya kuingia makubaliana na uongozi wa timu ya Coastal Union ambapo utiliaji saini huo ulishuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu wa Coastal Union, Kassim El Siagi, Meneja wa Coastal Union, Akida Machai na viongozi wengine.
Akizungumza mara baada ya kusaini, Chidiebele amesema kuwa amefurahi kusajiliwa na Coastal Union na kuhaidi kutumia uwezo wake aliokuwa nao kwa ajili ya kuipa mafanikio timu hiyo katika michuano ya Ligi kuu msimu ujao.

Wednesday, June 17, 2015


Ripoti toka England zimedai Manchester United wameshaanza mazungumzo na AS Monaco ili wamsaini Beki wa Brazil Fabinho.
Huku Fulbeki huyo akitaka kuhama, Monaco imeripotiwa kulikataa Dau la Pauni Milioni 10 la Man United na kutaka walipwe mara mbili.
Wakati huo huo, inasemekana Man United imemchukuwa Wakala kabambe, Jorge Mendes, ambae ndie huwasimamia Masupastaa kama Cristiano Ronaldo, Jose Mourinho na kadhalika, ili kuwasaidia kukamilisha Dili ya kumnasa Beki Nicolas Otamendi ambae Klabu yake Valencia inang'ang'ania kulipwa Pauni Milioni 35.
Nao Southampton wameiambia Man United kulipa Pauni Milioni 24 ikiwa wanataka kumnunua Kiungo mahiri Morgan Schneiderlin mwenye Miaka 25.

Hadi sasa Man United ndio wako mbele ya Arsenal katika mbio za kumnasa Kiungo huyo kutoka France ambae aliwika kwenye Ligi Kuu England Msimu uliopita.
Hadi sasa Meneja wa Man United, Louis van Gaal amefanikiwa kumnunua Winga wa Holland na PSV Eindhoven, Depay Memphis, ambae ndie Mfungaji Bora wa Ligi Kuu huko Holland.
Depay tayari alishatua Old Trafford


BAO za England zimefungwa na Karen Carney kipindi cha kwanza dakika ya 15 na lile la mkwaju wa penati dakika ya 38 la Fara Williams na kwenda mapumziko England wkiwa mbele ya bao 2-0 dhidi ya Wakolombia. 
Bao la Colombia lilifungwa na Lady Andrade (Colombia) dakika majeruhi dakika ya 90 na mtanange kumalizika kwa 2-1 England wakiibuka kidedea.Karen Carney akipongezwa baada ya kuifungia England bao la kwanza


TIMU ya Taifa ‘Taifa Stars’ leo asubuhi ilionja adha ya kuzomewa na mashabiki kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam ilipokwenda kufanya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa ma mchezo wa kufuzu fainali za kombe la mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) dhidi ya Uganda.
Taifa stars iliwasili uwanjani hapo saa 3:30 asubuhi na kukuta mashabiki wakiangalia mazoezi ya Yanga ambayo inajiandaa na mashindano ya Kagame yanayotarajia kuanza Julai, 9.
Baada ya kuwasili meneja wa timu hiyo Boniface Clemence alianza kushusha vifaa vya mazoezi na wachezaji kuanza kushuka, mashabiki walipowaona ndipo wakaanza kupiga kelele za kuzomea huku wengine wakiwaita watalii hali iliyofanya kocha kuamuru vifaa virudishwe ndani ya gari.
“Buuuh watalii hao, buuu watalii hao,” walizomea mashabiki hao.
Kelele hizo ziliongezeka kwani mashabiki waliokuwa kwenye jengo la Machinga nao walipowaona walizomea zaidi.
Baadae zomeazomea hiyo ilikuja kutulizwa na meneja Clemence pamoja msaidizi wa rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi Juma Matandika waliowataka mashabiki kuwa wazalendo kwani hiyo ni timu yao ya taifa hakuna haja kuizomea.

“Jamani mnapozomea haisadii kwani hii ni timu yetu sote watanzania ni kweli tumefungwa lakini angalia rekodi ya Misri, hakuna timu ambayo imekwenda kucheza pale ikatoka bila kufungwa tena kwa idadi kubwa ya mabao,”, alisikika akisema Clemence.
Baada ya hali kuwa shwari wachezaji na benchi la ufundi walitoka wakaingia Uwanjani kuanza mazoezi huku wakipishana na Yanga ambao nao walikuwepo kwenye Uwanja wa Karume wakifanya mazoezi.
Taifa stars inatarajiwa kuondoka leo kwenda visiwani Zanzibar kwa ajili ya mchezo dhidi ya Uganda utakaochezwa keshokutwa.


AFC Bournemouth vs. Aston Villa, Aug. 8
Manchester City vs Chelsea, August 15
Manchester United vs. Liverpool, September. 12
Chelsea vs. Arsenal, September 19Newcastle United vs Chelsea, September 26
Everton vs  Liverpool, October 3
Manchester United vs. Manchester City, Oct. 24
Sunderland vs  Newcastle United, Octoter 24
Arsenal vs  Tottenham, November 11
Chelsea vs  Manchester City, April 16

waliotembelea blog