Saturday, May 16, 2015

 Muonekano wa ndani wa ukumbi mpya wa mikutano uliojengwa na CCM mjini Dodoma ambao uko katika hatua za mwisho kukamilika kabla ya kuanza kutumika.Ukumbi huu upo karibu na jengo la  Benki Kuu, njia ya kuelekea Chuo Kikuu cha Dodoma - UDOM.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ujenzi wa Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Dodoma unaojengwa na  CCM.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ujenzi wa Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Dodoma unaojengwa na  CCM. Kulia ni makamu mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na makandarasi wanaojenga ukumbi wa kimataifa wa Mikutano wa Dodoma unaojengwa na  CCM, leo.Ukumbi huu upo karibu na Benki Kuu, njia ya kuelekea Chuo Kikuu cha Dodoma.

Muonekano wa ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Dodoma. Picha na Freddy Maro.


Steven Gerrard aliingia Uwanjani na Watoto wake wakati wa Mechi ya kumuaga rasmi leo Anfield.Wachezaji wenzake wa Liverpool wakimpa heshima Steven GerrardPicha ya PamojaSteven G. akiondoka Uwanjani na wanae tayari mchezo kuanza AnfieldHeshima kwa mkongwe Steven GerrardTaswiraBye bye Anfield!!Kila shabiki leo alikuwa na hamu kubwa ya kumuaga Steven Gerrard.Shujaa Steven GerrardTaswiara ya Uwanjani Anfield leo wakati wa kumuaga Kepteni Steven Gerrard.


RATIBA
Jumamosi Mei 16

14:45 Southampton vs Aston Villa
17:00 Burnley vs Stoke City
17:00 QPR vs Newcastle United
17:00 Sunderland vs Leicester
17:00 Tottenham vs Hull
17:00 West Ham vs Everton
19:30 Liverpool vs Crystal Palace
Jumapili Mei 17
15:30 Swansea vs Man City
18:00 Man United vs Arsenal
Jumatatu Mei 18
22:00 West Brom vs Chelsea
Jumatano Mei 20
2145 Arsenal vs Sunderland

Friday, May 15, 2015

KEPTENI wa Liverpool Steven Gerrard Jumamosi ataichezea Klabu yake kwa mara ya mwisho Uwanjani kwao Anfield na Tiketi za Mechi hiyo zimefika Bei ya Shilingi Milioni 4, 090, 680/=.
Jumamosi Liverpool watacheza Mechi yao ya mwisho ya Ligi Kuu England Msimu huu Uwanjani kwao Anfield dhidi ya Crystal Palace.


Hii Leo mtandao unaouza Tiketi kwa ajili ya Mechi hiyo, www.ticketbis.net umeanika Bei za Tiketi za kuanzia Pauni 100 hadi 1,324.64 ikiwa ni takriban Shilingi 314,727 hadi Shilingi 4,166, 985.

Kwa Mechi ya kawaida kwenye Jukwaa Kuu la Anfield Tiketi huuzwa Pauni 47 yaani Shilingi 147,922.
Gerrard, mwenye Miaka 34, anastaafu kuicheza Liverpool Msimu huu baada ya kuwa nao kwa Miaka 17 na Mechi yake ya mwisho kabisa itakuwa Wiki ijayo Ugenini wakicheza na Stoke City.
Hata hivyo, Gerrard ataendelea kusakata Soka huko Marekani akichezea Ligi ya MLS na Klabu ya LA Galaxy.
Zipo habari zinasema Gerrard atawekewa Gwaride la Heshima na WAchezaji kabla ya Mechi ya Jumamosi kuanza kati ya Liverpool na Crystal Palace.

 Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Dkt.Shukuru Kawambwa akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma  kuongoza sherehe za kilele cha wiki ya Elimu kitaifa Mei 15,2015. 
 Balozi wa Chini nchini Tanzania,Lu Youging akizungumza jambo na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma  kuongoza sherehe za kilele cha wiki ya Elimu kitaifa Mei 15,2015,kulia ni Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Mh.Anne Kilango Mallecela. 
 Baadhi ya Wanafunzi kutoka katika shule mbalimbali mjini Dodoma waliohudhuria sherehe za kilele cha wiki ya Elimu kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma Mei 15,2015 .

Wednesday, May 13, 2015


Cristiano Ronaldo akshangilia bao lake la PenatiDakika ya 23 kipindi cha kwanza Cristiano Ronaldo anaipachikia bao la kwanza Real Madrid kwa mkwaju wa Penati na kufanya 1-0 dhidi ya Juventus. Bao hilo la Cristiano Ronaldo lilidumu na kuwapeleka mapumziko wakiwa mbele  na huku jumla ya magoli ya mtanange wa kwanza na huu japo bado dakika ya 45 ikiwa ni (Agg 2-2).Wachezaji wa Juve wakimjia juu Mwamuzi wa mtanange baada ya kutokea penatiRonaldo chini akiutafuta mpira!
VIKOSI:
Real Madrid wanaoanza:
Casillas, Carvajal, Varane, Sergio Ramos, Marcelo, Rodriguez, Isco, Kroos, Bale, Benzema, Ronaldo
Real Madrid Akiba: Navas, Pepe, Fabio Coentrao, Hernandez, Arbeloa, Jese, Illarramendi
Juventus wanaoanza: Buffon, Lichtsteiner, Bonucci, Chiellini, Evra, Marchisio, Pirlo, Pogba, Vidal, Tevez, Morata
Juventus akiba: Storari, Coman, Llorente, Barzagli, Padoin, Sturaro, Pereyra

waliotembelea blog