Friday, April 10, 2015



DSC_0616
Aneth Kushaba AK 47(katikati) akiimba na waimbaji wenzake wa bendi ya Skylight ambao ni Ashura Kitenge(kushoto) na kulia ni John Music kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower akiimba na kucheza moja ya Sebene la Kikongo pamoja Sony Masamba.
Sony Masamba ambaye ni mmoja wa waimbaji wa Skylight akiendelea kutoa burudani huku akisindikizwa na waimbaji wenzake kulia ni Sam Mapenzi na kushoto ni Joniko Flower
Waimbaji wa Skylight Band wakiimba kwa moja ya nyimbo za bendi yao kwenye kiota cha Thai Village ijumaa iliyopita.

Sugua sugua mpaka itakate……Waimbaji wa Skylight Band wakicheza moja ya style zao zinazobamba mujini.
Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK 47 akiimba sambamba na msanii mwenzake Sam Mapenzi kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar
Burudani ikiendelea kutolewa na wasanii wa Skylight Band.
Ashura Kitenge akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band huku akisindikizwa na Aneth Kushaba AK 47(kushoto) pamoja na John Music (kulia)
Ashura Kitenge akiimba kwa hisia pamoja na Sam Mapenzi mbele ya mashabiki wa Skylight Band(hawapo pichani) kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar
Sugua Sugua mpaka utakate njoo leo ujifunze kusugua kama hawa mashabiki wa Skylight walivyojua mmoja ya Style ya kusugua
Sam Mapenzi akiendelea kutoa burudani kwa mashabiki wa Skylight band (hawapo pichani) huku akisaidiwa na waimbaji wenzake wa kwanza kushoto ni Ashura Kitenge akiwa smambamba na Sony Masamba(wa pili kutoka kushoto) pamoja na John Music (wa kwanza kulia) kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein akikabidhiwa Jezi ya Bacelona namba 14 ya mchezahji wa zamzni akiwa kocha Johan Cruyff (kushoto)wakati wa hafla fupi ya chakula jioni  iliyofanyika jana Ikulu Mjini Zanzibar timu hiyo ilipokutana na Rais.[Picha na Ikulu) CRU2


Robin van Persie amejitangaza kuwa yupo vizuri kwa mchezo wa jumapili dhidi ya wapinzani wao wa jadi Manchester city.
Van Persie amekosekana michezo sita ya Manchester united kutokana na kuumia enka wakati Man Utd walipopoteza kwa 2-1 dhidi ya Swansea tarehe 21 mwezi wa pili.

Kocha Louis van Gaal wiki iliyopita alisema hakutegemea Van Persie kupona kwa haraka hivyo na kua vizuri kupambana na city jumapili ijayo pale Old Traffod,lakini Van Persie mwenyewe alijitangaza kwa mashabiki na kuwaambia yupo vizuri.
Hata kama van Gaal akifikiria kumpa nafasi katika mechi yao ya upinzani wa jadi dhidi ya city bado ni ngumu sana kuona jinsi gani ataendana na kasi na mfumo wa sasa ya kitika kikosi cha kwanza
Pengo la mholanzi ambae amefunga magoli 10 tu msimu huu halikuonekana kabisa pale alipoumia,na tangu alipoumia man united imepoteza mchezo mmoja tu tena dhidi ya mabosi wake wa zamani Arsenal kombe la FA.

United walipata ushindi katika ratiba ngumu dhidi ya Tottenham na Liverpool na jumamosi iliyopita ushindi wa 3-1 dhidi ya Aston Villa ushindi uliofanya kuwa juu ya city kwa pointi moja.
Wayne Rooney alifunga goli moja matata kwa mkwaju wa haja,kapteni huyo wa united amekua na kiwango bora kabisa pale mbele katika mfumo wa 4-3-3 akisaidiana na Ashley Young na Juan Mata ambae aliingia nyavuni mara mbili katika ushindi wa 2-1 pale Anfield wiki mbili na nusu zilizopita.
Marouane Fellaini pia anatoa mchango mkubwa katika majukumu ya kiungo na ushambuliaji sehemu ambayo kwa sasa imetulia sana kwenye kikosi hicho cha Manchester united.
 Ushindi dhidi ya city iliyopoteza mwelekeo na kuwa chini ya kiwango utaongeza wigo wa pointi kufikia nne na kuongeza matumaini ya Van Gaal kucheza ligi ya mabingwa msimu ujao.Mata na Ander Herrera

Thursday, April 9, 2015


MENEJA wa Chelsea Jose Mourinho ameusapoti msimamo wa Arsene Wenger kwamba Ballon d'Or ifutiliwe mbali
Mwezi Januari, Wenger, ambae ni Meneja wa Arsenal, aliiponda Tuzo hiyo ya FIFA anaetunukiwa Mchezaji Bora Duniani wa Mwaka na kusisitiza kuwa angepewa nafasi ya kupiga Kura asingekubali.

Hata hivyo, Wenger hana nafasi ya kumpigia Kura Mgombea wa Tuzo hiyo kwa vile Washiriki wake ni Makocha wa Timu za Taifa na Manahodha wake pamoja na Jopo maalum la Wanahabari.
Cristiano Ronaldo, ambae aliwahi kucheza chini ya Mourinho alipokuwa Real Madrid, ndie anaeshikilia Tuzo hiyo kwa sasa baada ya kuitwaa kwa mara ya 3 Mwezi Januari.

Akiongea hapo jana, Mourinho alisema Tuzo hiyo inavuruga Soka kwa kuweka msisitizo kwa Mtu binafsi badala ya Timu.
Mourinho alisema: "Nadhani Wenger alisema kitu cha maana, anapinga Ballon d’Or, na nadhani yuko sahihi kwa sababu kwa sasa Soka linapoteza mvuto wa Kitimu na kutilia mkazo Mtu binafsi!"
Mourinho alinena: "Sasa tunatizama ubinafsi. Fulani na takwimu zake kwamba alikimbia umbali mrefu. Kwa sababu kwenye Gemu umekimbia Kilomita 11 na mie nimekimbia 9 wewe ndio umefanya kazi nzuri? Pengine siyo! Labda Kilomita zangu 9 ni muhimu kuliko zako 11! Kwangu mie Soka ni Kitimu. Mtu binafsi anakaribishwa ikiwa anataka kufanya Timu yetu iwe bora!''
Aliongeza: "Mchezaji mkubwa akiwasili anaikuta Timu ipo. Si yeye anaeigundua Timu kama vile Columbus alivyoivumbua Amerika. Wewe unakuja kutusaidia tuwe bora zaidi. Kama Meneja kila Siku inabidi utoe ujumbe huu!"

FIFA Leo hii imetoa Listi ya Ubora Duniani kwa Nchi na Mabingwa wa Dunia Germany wameendelea kuwa juu wakifuatiwa na Argentina huku Tanzania ikishuka Nafasi 7 na kushika Nafasi ya 107.
Nchi ya juu kabisa kwa Afrika bado ni Algeria lakini imeporomoka Nafasi 3 na sasa ipo ya 21 ikifuatiwa na Ivory Coast ambayo pia imeshuka Nafasi 3 na ipo ya 23.
Nchi mpya kwenye 10 Bora ni Switzerland na Spain wakati France na Italy zimetoka huko.

Nayo Belgium imepanda Nafasi 1 na ni wa 3 baada ya kuchukua nafasi ya Colombia huku Brazil wakipanda moja wakiwa Nafasi ya 5.
England nao wanaisogelea 10 Bora baada kupanda Nafasi 3 na kushika Nafasi ya 14.
Listi nyingine ya Ubora itatolewa hapo Mei 7

LISTI YA UBORA DUNIANI:
20 BORA:

1. Germany
2. Argentina
3. Belgium
4 Colombia
5. Brazil
6. Netherlands
7. Portugal
8. Uruguay
9. Switzerland
10. Spain
11. France
12. Romania
13. Italy
14. England
15. Costa Rica
16. Chile
17. Croatia
18. Mexico
19. Czech Republic
20. Slovakia


Real Madrid inazidi kuipumulia Barcelona katika mbio za La Liga baada ya kuichapa Rayo Vallecano 2-0 Kwa ushindi huo, Real Madrid inaendelea kutofautishwa kwa pointi kati yake na Barcelona ambayo hapo awali iliifumua Almeria 4-0. Ronaldo akishangilia bao lake la 300Mabao ya Real Madrid yamefungwa na Cristiano Ronaldo aliyetupia katika dakika ya 68 muda mfupi baada ya kulimwa kadi ya njano kwa kujirusha huku bao la pili likifungwa na James Rodriguez dakika ya 74.
DSC_0377 


  DSC_0338 DSC_0379 
  DSC_0387 DSC_0404 
  DSC_0301 DSC_0406 
  DSC_0386 DSC_0368
DSC_0219 


DSC_0226 

DSC_0235
DSC_0274

waliotembelea blog