Thursday, August 28, 2014

Crystal Palace imemteua Bosi wao wa zamani Neil Warnock kama Meneja wao mpya.
Warnock, mwenye Miaka 65 na ambae alikuwa Palace kati ya Mwaka 2007 na 2010, amesaini Mkataba wa Miaka Miwili.
Mkongwe huyo mwenye makeke na vituko anachukuwa wadhifa kutoka kwa Tony Pulis ambae alibwaga manyanga Masaa 48 tu kabla Msimu mpya wa Ligi Kuu England kuanza hapo Agosti 16.
Msimu uliopita, Tony Pulis, aliteuliwa kuwa Meneja wa Msimu wa Ligi Kuu England baada ya kuiongoza Palace kutoka mkiani wakati akishika wadhifa huo kutoka kwa Ian Holloway Mwezi Novemba 2013 na kumaliza Ligi ikiwa Nafasi ya 11.
Warnock amekuwa hana kazi tangu Aprili 2013 alipoachana na Klabu ya Leeds United.

Kurudi kwa Warnock kumeleta mvuto hasa kufuatia tukio la Winga wa Klabu hiyo, Jason Puncheon, kupandwa ghadhabu na kubatuka kwenye Mtandao wa Twitter akimponda Warnock ambae, wakati akiwa Mchambuzi kwenye TV, alimkosoa Puncheon kwa kukosa Penati na tukio la Puncheon kutoa maneno makali kwenye Twitter liliifanya FA imtwange Mchezaji huyo Faini ya Pauni 15,000.

Mwaka 2010, Warnock aliondoka Palace baada ya Klabu hiyo kuwekwa chini ya Mwangalizi maalum ili kuepuka kufilisiwa, kitendo ambacho kiliifanya Klabu hiyo ikatwe Pointi 10 na kuiweka kwenye hali ngumu na nusura ishushwe kutoka Daraja la Championship.

Choices: Co-chairman Steve Parish has been looking for a new manager since Tony Pulis left earlier this month
Mwenyekti msaidizi Steve Parish alikuwa akitafuta Kocha mpya tangu Tony Pulis atimke zake Klabuni hapo.
Manager: Neil Warnock previously managed Crystal Palace between 2007-10, but left to join QPR
Neil Warnock pia alishaiongoza Crystal Palacekati ya mwaka 2007-10, lakini pia alioongoza QPR

Wednesday, August 27, 2014


Photo: 'United are the only club I could have left Madrid for': Di Maria signs five-year deal at Old Trafford to smash British transfer recordAngel di Maria Akiwa amebeba jezi yake leo hii wakati anasaini mkataba na Klabu yake mpya ya Man United leo. Angel di Maria ametokea katika Ligi ya Spain kwenye timu ya Real Madrid.
Got him! Angel di Maria poses with Manchester United boss Louis van Gaal upon signing
Angel di Maria akiwa kwenye picha ya pamoja na Bosi wake Mpya wa  Manchester United Louis van Gaal
New motor: Di Maria poses in front of a Chevrolet car outside Aon Training Complex
Di Maria akiwa na Gari aina ya Chevrolet nje ya Uwanja wa mazoezi Aon Complex
Long-term man: Di Maria signs on a five-year deal from European champions Real Madrid
Di Maria amesaini Mkataba wa miaka 5.
MANCHESTER UNITED imetangaza rasmi kuwa Angel Di Maria amekamilisha Uhamisho wake kwa Dau la Rekodi huko Uingereza la Pauni Milioni 59.7 akitokea Real Madrid ya Spain.
Mara baada ya kukamilisha taratibu za Uhamisho, Di Maria alisema: “Nina furaha kupita kifani kujiunga na Manchester United. Nilikuwa na raha kule Spain na Klabu nyingi zilinitaka lakini Man United ndio Klabu pekee ningeweza kuiacha Real Madrid ili kujiunga nayo.
Louis van Gaal ni Kocha bora sana mwenye rekodi nzuri na nimevutiwa mno na dira na nia ya kila Mtu Klabuni hapa ili kuirudisha tena juu ambako ndiko inastahili kuwepo. Nani hamu kubwa kuanza kazi!”

Nae Meneja Louis van Gaal, akimkaribisha Di Maria, amesema: “Angel ni Kiungo wa kiwango cha Dunia lakini muhimu zaidi ni Mchezaji Kitimu. Hamna shaka kuhusu kipaji chake kisicho mfano. Ni mwepesi sana na hatari kwa Guu la Kushoto ambae anatisha Difensi yoyote ile. Uwezo wake kukokota Mpira na kuwakabili Mabeki na kuwadaa ni kitu cha furaha kukiangalia. Ni nyongeza safi sana kwa Timu!”
Chief coup: Executive vice-chairman Ed Woodward poses with Di Maria
Di Maria akimwaga wino kusaini Mkataba na Klabu ya Man United na hapa alikuwa na Mwenyekiti wa Klabu hiyo Ed Woodward.

Monday, August 25, 2014



Wakongwe wa Klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania wakipiga picha za kikundi cha ngoma kilichokuwa kikiwatumbuiza mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro kabla ya kuelekea Mlima Kilimanjaro.

Wachezaji wakongwe wa Klabu ya Real Madrid wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa TANAPA mara baada ya kumaliza zoezi la matembezi mafupi ya kupanda Mlima Kilimanjaro.

Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Dk. Fenela Mukangara akitoa cheti cha ushiriki kwa mchezaji Ruben De La Red wa Klabu ya Real Madrid mara baada ya kumaliza zoezi la matembezi mafupi ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete akikabidhi moja ya fulana za TANAPA kwa mchezaji.
Tafrija ya kuwaaga kabla ya kupanda mlima ikiendelea.

wakali hao wa zamani wa Real Madrid wakiwa katikati ya msitu wa Mlima Kilimanjaro.

Eneo la Maporomoko ya Maji ambapo wachezaji wakali hao wa zamani wa Real Madrid walifanikiwa kufika Mlimani Kilimanjaro.

Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete (mwenye fulana nyeupe na miwani) akiongoza msafara wa wakali hao wa zamani wa Real Madrid kukwea Mlima Kilimanjaro.



Di Maria akiingia kwenye imaya ya Man United kwenye sehemu yao ya Mazoezi

Di Maria kwenye siti ya nyuma akiingia

Di Maria Anaungana na Marcos Rojo, Ander Herrera pamoja na Luke Shaw ambao ndio tayari wamesainiwa na Man United Msimu huu wa 2014/15


Stevan Jovetic akishangilia bao lake dakika ya 55 kipindi cha pili.
Ni Stevan Jovetic huyo hyo ndie kazichana nyavu tena kwa kufunga bao la pili dakika ya 55 baada ya kupata pasi kutoka kwa Samir Nasri. Bao la tatu lilifungwa na Sergio Agüero dakika ya 69  kipindi cha pili baada ya kupata ushirikiano safi kutoka Jesús Navas González. Bao la Liverpool lilipatikana dakika ya 83 na ni la kujifunga wao wenyewe kupitia kwa Pablo Zabaleta.Aguero akifunga bao lake na kufanya 3-0 dhidi ya Liverpool.Asantee!Kipindi cha kwanza kikiendelea...
City Wanaongoza kwa bao 1-0 dhidi ya Liverpool, Bao likifungwa na Stevan Jovetic dakika ya 41.

Mario Balotelli kauangalia mtanange huu kati ya Manchester City vs Liverpool kama shabiki!

Balotelli akiwa na Adam Lallana wakiutazama mchezo huu kwenye uwanja wa Etihad huku Kocha wa zamani wa Liverpool Kenny Dalglish nae akiwa mbele yao akiuchabo mpira huo.

Mario kajiunga rasmi leo na Liverpool baada ya kukamilisha uhamisho wake kurudi England na huu ndio mtanange wake wa kwanza kuuangalia japo hakucheza.


BenzemaBenzema aanza kufungua lango...1-0 Bao hilo lilifungwa dakika ya 30 kipindi cha kwanza.
Bao la pili limefungwa na Cristiano Ronaldo katika dakika za majeruhi dakika 90 baada ya kuachia shuti kali lililomzidi ujanja kipa wa Cordoba.
Ronaldo kwenye patashika..

Ronaldo chini akilalamika!Bale akimiliki mpira..huku akinyemelewa na Matos wa Cordoba

Waendeshaji wa Kipindi cha Filamu Monata kinachorushwa na Kituo cha Redio cha TIMES FM 100.5 wakiendelea na majukumu katika studio za kituo hiko cha Redio Kilichopo Kawe Jijini Dar Es Salaam wakati wa Kipindi cha Filamu Monata leo wakati washiriki 10 Bora wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) walipotembelea Studio hizo 
Jaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) na Presenta wa Kipindi cha Filamu Monata cha TIMES FM, 100.5 Dar Es Salaam akiendelea na kipindi wakati washiriki 10 bora walipotembelea Kituo hiko leo kwaajili ya Mahojiano na waendeshaji wa Kipindi hiko.
 Mmoja wa Washiriki 10 Bora wa Tanzania Movie Talents (TMT) akijibu maswali kutoka kwa Waendeshaji wa Kipindi cha Filamu Monata kinachorushwa na Kituo cha Redio cha TIMES FM, 100.5 Dar Es Salaam.
Mshiriki Wa Tanzania Movie Talents (TMT) akijibu maswali.
 Washiriki 10 Bora wa Tanzania Movie Talents (TMT) wakiwa ndani ya Studio za TIMES FM, 100.5 Dar es Salaam.Picha Zote na Josephat Lukaza

Fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) kufanyika tarehe 30 August 2014 katika Ukumbi wa Mlimani City kuanzia Saa 7.30 Usiku huku viingilio vikiwa Shilingi elfu 50 kwa VIP na Elfu 30 kwa kawaida

Burudani Kali kutolewa siku hiyo ya Fainali Huku Mc Pilipili akitoa burudani na Christian Bella

waliotembelea blog