Sunday, August 10, 2014


 
Mwanza umekua ndiyo mkoa wa kwanza kufungua shamra shamra hizi za Fiesta kwa mwaka 2014 ambapo on stage zaidi ya wasanii 15 walipata nafasi ya kushow love na wakazi wa Mwanza kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
 Inawezekana show hii ikaingia kwenye list ya miongoni mwa show zilizowahi kuhudhuriwa na wakazi wengi sana wa jiji hili la Mwanza kwa sababu nilipata taarifa kuwa ilipofika saa 5 tu usiku tiketi zote zilikuwa zimeisha.




 Ukiachilia mbali wasanii waliokuwa wakitajwa kwenye matangaazo kulikuwa na SAPRAIZ nyingine kwenye jukwaa la Fiesta,Mwanza walimuona Jokate akiimba kwa mara ya kwanza kwenye jukwaa na kushangiliwa sana kutokana na alivyoifanya show hiyo.















 




IMG-20140809-WA009
Timu ya Kivule veterani ya jijini Dar es salaam kwenye picha ya pamoja kabla ya kuvaana na timu ya Namanga veteran kwenye uwanja wa Sheikh Amri Kaluta Abeid jijini Arusha
Mahmoud Ahmad Arusha
Timu ya Ushirika Veteran ya mkoani Kilimanjaro imeibuka bingwa wa Bonanza la Nanenane kwa kuifunga timu ya Kivule veteran ya ukonga jijini Dar es salaam kwa magoli 3-0  katika mchezo wa fainali ya mashindano hayo yaliondaliwa na timu ya Arusha All Stars kwenye uwanja wa sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
 
Michezo hiyo ya nanenane iliyozishirikisha timu kutoka mikoa ya Arusha,Dodoma, Mwanza,Dar es salaam na Kilimanjaro ambao timu yao ndio waliibuka mabingwa wa mashindano hayo kwa timu za ushirika veteran na kivule kucheza fainali
 
Hata hivyo wenyeji wa mashindano hayo waliambulia nafasi ya nne baada ya kufungwa katika mechi ya kugombea nafasi ya tatu na timua ya Dodoma veteran iliyokuwa inaongozwa na mkongwe wa soka hapa nchini Charles Mgodo.
 
Akizungumza baada ya mechi hiyo mgodo aliwataka wachezaji wa sasa kuangalia michezo ya maveterani katika mabonanza mbalimbali kwani watajifunza kitu kutoka kwao ikiwemo nidhamu ya michezo na kujituma kama walivyoonyesha baadhi ya wachezaji wa miaka ya nyuma wa timu zilizotamba kwenye ligi kuu.
 
Pia Mgodo alisema kuwa maandalizi ya timu za vijana wa sasa na wazamani ni tofdauti huku akisema kuwa vijana wa sasa wanataka kucheza kama mchezaji Fulani baada ya kuangalia tv huku hawajitumi hili ni tatizo na kuwataka kuanza kujituma na kutoweka maslahi mbele na kuuvaa uzalendo.
 
Akalishauri shirikisho la michezo hapa nchini Tff kurudi mashuleni au kuanzisha Academy ilkuweza kuibua vijapaji na sio kuviacha vikielea bila ya kuviendeleza hili ni tatizo kwa ukuaji wa michezo hapa nchini.
 
“Tunataka vijana wakija kwenye mabonanza waje kujifunza mpira na kuangalia tofauti ya mpira wanaocheza wao na wa wazee wao hapa umeona wachezaji wa zamani wakijituma tokea mwanzo wa mchezo hadi mwisho na wao wanatakiwa kuwa kama hivi ila kikubwa wawe wazalendo kwa taifa lao hapo tutafanikiwa”alisema Mgodo.


Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji na viongozi wa Simba pamoja na Rais wa TFF, Jamal Malinzi. (Picha na Francis Dande)

Kikosi cha Simba kikiwa na Kocha Mkuu, Zdravko Logarusic (kulia), pamoja na Rais wa Simba, Evans Aveva.

Kikosi cha Zesco.

Ramadhani Singano 'Mess' akiwatoka wachezaji wa Zesco.

Mshambuliaji wa Simba, Raphael Kiongera (kushoto), akimtoka beki wa Zesco United ya Zambia, Bernad Mapili katika mchezo maalumu wa kirafiki wa kimataifa wa Simba Day uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Zesco ilishinda 3-0.
Golikipa wa Zesco, Lameck Nyangu akiokoa moja ya hatri zilizoelekezwa langoni mwake.

Amis Tambwe akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Zesco, Bernad Mapili.

Mshambuliaji wa Ismba, Issa Rashid akichuana na beki wa Zesco.


Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Haasan Dalali akitambulishwa.

Crescentius Magori akitambulishwa jukwaa Kuu.

Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima akipeana mkono na Ivo Mapunda.

Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima akiwa amepozi katrika picha na kipa wa Simba, Ivo Mapunda.

Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima akisalimiana na Mshambuliaji wa Simba, Raphael Kiongera.

MC akiongoza sherehe za Simba Day.

Timu zikiingia uwanjani.

Wachezaji wakiingia uwanjani.

Benchi la ufundi la Zesco.

Timu za Simba na Zesco kabla ya mchezo.

Tunawakilisha.

Twanga Pepeta wakitoa burudani.

Mashabiki wa Simba wakiwa hawaamini kilichotokea uwanjani baada ya kufuungwa mabao 3-0 na Zesco.

Wanenguaji wa Twanga Pepeta wakitumbuiza wakati wa mechi ya Simba na Zesco ya Zambia.
Beki wa timu ya zesco, Zimisileni Moyo (juu) akichuana na mshambuliaji wa simba, Oasainou Manneh, kuwania mpira wakati wa mchezo wa kirafiki katika Tamasha la Simba Day,lililofanyika leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Katika mchezo huo Simba ilikubari kichapo cha mabao 3-0.

Amri Kiemba wa simba (kulia) akimtoka Clatous Chama, wakati wa mchezo huo.



Beki wa simba William Lucian (katikati) akimtoka mchezaji wa Zesco, Winston Kalengo,wakati wa mchezo huo.



Mwimbaji wa bendi ya Twanga Pepeta, Kaalala Junior, akiimba wakati bendi hiyo ilipokuwa ikitoa burudani katika Taamasha hilo.



Kalala akiwachezesha wanenguaji wake.



Wanenguaji wa Twanga, wakishambulia jukwaa.



Wanamuziki wa twanga wakiimba uwanjani hapo..



Sehemu ya mashabiki wa Simba waliohudhuria Tamasha hilo.



Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Barnaba, akiimba uwanjani hapo wakati wa Tamasha hilo.

waliotembelea blog