Tuesday, May 6, 2014


Mtaalamu wa nyasi bandia kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Ian McClements amewasili Bukoba leo hii Asubuhi kwa Ndege ya kukodi. 
McClements akiwa hapa Bukoba amekagua Uwanja wa Kaitaba, na baadae amekwea tena ndege yake kuelekea  jijini Mwanza kukagua Uwanja wa Nyamagana.




Viwanja hivi vinawekwa nyasi bandia kwa ufadhili wa FIFA chini ya mpango wa misaada wa Goal Projects. Baada ya ukaguzi huo, McClements atatuma ripoti yake FIFA ili shirikisho hilo liweze kuteua mkandarasi wa kufanya kazi hiyo.
Kwa Tanzania viwanja vilivyowekwa nyasi bandia hadi sasa kupitia Goal Project ni Uwanja wa Uhuru uliopo Dar es Salaam, Uwanja wa Karume (Dar es Salaam) na Uwanja wa Gombani uliopo Pemba.

Dr. Ian McClements (kulia) akipata maelekezo kutoka kwa Eng. George Geofrey wa Manispaa hapa Bukoba
Dr. Ian McClementsNje kidogo ya mipaka ya Uwanja Dr. Ian McClements analazimika kuchimba ili aweze kuona chini kuna nini? akitaka kupima maji yanafyonzwa vipi na ni udongo gani? na Je Maji yananyonywa vipi na udongo wa hapa Kaitaba ususani kwenye uwanja huu huu wanaotaka kuuwekea nyasi za Bandia.
Dr. Ian McClementsKumbe kuna mchanga chini, yes! safi
Dr. Ian McClements (kulia) akichukua kumbukumbu kushoto ni Eng. George Geofrey wa Manispaa hapa Bukoba.
Dr. Ian McClement akipima kina
Dr. Ian McClement alimwaga maji ndani ya shimo ili kuona kaji nini kitafata na je yatanyonywa na udongo kwa muda gani!

Ili chukua muda wa dakika 1 na sekunde 40 tu maji yalikuwa yameishatowekaAkipima maji aliyoweka
Dr. Ian McClements akichukua maelezo kutoka kwa Eng. George Geofrey wa Manispaa hapa Bukoba
Alichima na sehemu ya upande wa pili wa goli



Dr. Ian McClements akiteta jambo na Kiongozi Katibu wa KRFA Jumanne Chama

Hapa mchanga hakuna na Udongo wake ni Mweusi mchanga upo chini zaidi

 


Dr. Ian McClements baada ya kumaliza kazi yake alipaa kuelekea jijini Mwanza na hapa alikuwa anaagana na Jumanne Chama kwenye Uwanja wa Ndege
Mwewe yupo tayari!



Afisa Tarafa wa Moshi mjini, William Issa(wa pili kushoto) akimkabidhi kikombe Nahodha wa timu ya Chuo cha RUCCO cha Iringa, Said Mohamed mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za kitaifa za “Safari Higher Learning Pool Competition 2014” zlizomalizika mwishoni mwa wiki mjini Moshi.Wa pili kulia ni Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akishangilia na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Pool Taifa, Fred Mushi(kushoto).

Afisa Tarafa wa Moshi mjini, William Issa(wa pili kushoto) akimkabidhi kikombe Nahodha wa timu ya Chuo cha RUCCO cha Iringa, Said Mohamed mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za kitaifa za “Safari Higher Learning Pool Competition 2014” zlizomalizika mwishoni mwa wiki mjini Moshi.Kulia ni Betrice Madafu kutoka chuo hicho akwa ameshikilia kitita cha fedha taslimu Shilingi 2,500,000/=,Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akishangilia na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Pool Taifa, Fred Mushi.

Afisa Tarafa wa Moshi mjini, William Issa(kushoto) akimkabidhi Nahodha wa timu ya Chuo cha RUCCO cha Iringa, Said Mohamed kitita cha fedha taslimu Shilingi 2,500,000/= mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za kitaifa za “Safari Higher Learning Pool Competition 2014” zlizomalizika mwishoni mwa wiki mjini Moshi.Kulia ni Betrice Madafu kutoka chuo hicho na katikati ni Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.

Wachezaji wa timu ya Chuo cha RUCCO cha Iringa wakishangilia na kikombe pamoja na fedha taslimu Shilingi 2,500,000/= mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za kitaifa za “Safari Higher Learning Pool Competition 2014” zilizomalizika mwishoni mwa wiki mjini Moshi.RUCCO waliupata ubingwa huo kwa kukifunga chuo cha St. John 13-12.

RUCCO Iringa mabingwa wa Taifa Safari Pool 2014.
Na Mwandishi Wetu.Moshi
CHUO cha RUCCO cha mkoani Iringa kimefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya mchezo wa Pool Taifa yaliyoyoshirikisha mabingwa wa Vyuo vya Elimu ya juu kutoka mkoa minane yajulikanayo kama “Safari Pool Higher Learning Competition 2014” mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Aventure Moshi -Kilimanjaro. 

 RUCCO Iringa mabingwa wa Taifa Safari Pool 2014.
Na Mwandishi Wetu.Moshi
CHUO cha RUCCO cha mkoani Iringa kimefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya mchezo wa Pool Taifa yaliyoyoshirikisha mabingwa wa Vyuo vya Elimu ya juu kutoka mkoa minane yajulikanayo kama “Safari Pool Higher Learning Competition 2014” mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Aventure Moshi -Kilimanjaro. RUCCO ilifanikiwa kupata ubingwa huo kwa kukifunga chuo cha St. John cha Dodoma 13-12, na hivyo kuzawadiwa kikombe na fedha taslimu Shilingi 2,500,000/=


Nafasi ya pili ilichukuliwa na St. John ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi 1,500,000/=,nafasi ya tatu ilichukuliwa na chuo cha Ardhi cha Dar es Salaam kwa kukifunga chuo cha Muccobs 13-8 na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi 1,300,000/= na nafasi ya nne ikaenda kwa wenyeji wa mashindano hayo Muccobs ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi 1,000,000/=


Timu zingine ambazo hazikufanikiwa kufikia hatua ya nne bora zilizawadiwa kifuta jasho cha fedha taslimu shilingi 500,000/= kwa kila chuo ambavyo ni chuo cha TIA,Bugando,Sua na Mzumbe.


Upande wa mchezaji mmoja mmoja Wanaume,Fredrich Mwangata kutoka chuo cha SAUT Mwanza alifanikiwa kutwaa ubingwa wa Taifa na kuzawadiwa Ngao pamoja na fedha taslimu Shilingi 300,000/= kwa kumfunga Steven Kyasi kutoka Chuo cha Mzumbe Mbeya 4-0,ambaye alichukua nafasi ya pili na kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi 200,000/=


Nafasi ya tatu ilichukuliwa Justus Mhando kutoka chuo cha Mipango Dodoma ambaye alizawadiwa Shilingi 150,000/= na nafasi ya nne alichukua Ally Jamson wa Muccobs Moshi na kuzawadiwa 100,000/=.


Upande wa kinadada Jacline Molel kutoka chuo cha TIA alitwaa ubingwa wa Taifa na kuzawadiwa ngao pamoja na fedha taslimu Shilingi 200,000/= kwa kumfunga Deborah Ramadhani kutoka chuo cha SILA Arusha 3-0 na hivyo Debora kushika nafasi ya pili na kuzawadiwa Shilingi 150,000/=. Nafasi ya tatu ilichukuliwa na Rehema Uzi kutoka Chuo cha UDOM ambaye alizawadiwa Shilingi 100,000/= na nafasi ya nne ilichukuliwa na Beatrice Madafu kutoka RUCCO ambaye alizawadiwa Shilingi 50,000/=


Fainali za Kitaifa zilishilikisha mikoa nane ambayo ni Iringa, Mbeya, Morogoro, Dodoma, Mwanza, Dar es Salaam, Arusha na wenyeji wa mashindano wa mwaka huu wa 2014,Mkoa wa Kilimanjaro.



Wachezaji wa Crystal Palace wakiwa kwenye uwanja wao wamekamua vilivyo na kuweza kuweka heshima kutoka kwenye kichapo cha bao 3-0 na kusawazisha kwa kufanya 3-3 na kuwapoteza uelekeo kileleni Liverpool. Ubingwa kwao sasa ni Miujiza!!! Huku wakiwa na mtanange mmoja tu wa jumapili ijayo na Newcastlw United.GayleMajogoo yachafuliwa mbio za Ubingwa na  Crystal Palace usiku huu kwa sare ya hatari. wakiwa mbele ya bao 3-0 na bao zote kurudi na kufanya sare ya 3-3.Can't even look: Reds talisman Suarez breaks down after his side shipped a 3-0 lead
Usiku huu Liverpool wamerejea kuongoza Ligi Kuu England wakiwa Pointi 1 mbele ya Manchester City kwa kucheza Mechi 1 zaidi licha ya kuumwaga uongozi wa Bao 3-0 na kuiruhusu Crystal Palace kurudisha Bao zote 3 ndani ya Dakika 8 za mwisho wa Gemu.

Captain Steven Gerrard....hoi!!!

Bao za Liverpool zilifungwa na Allen, Sturridge na Suarez na Palace kuchachamaa na kurejesha Bao hizo ndani ya Dakika 8 kuanzia Dakika ya 81 kwa Delaney kufunga Bao 1 na Dwight Gayle Bao 2.
Matokeo haya yamewabakisha Chelsea kwenye kinyang’anyiro cha Ubingwa pamoja na Liverpool na Man City lakini ni wazi City, wenye Mechi 2 mkononi, Ubingwa uko mikononi mwao wenyewe.

Suarez hoi!!! ni machozi!! Wakiwa wana bao tatu mkononi Liverpool usiku huu wamelazimishwa sare ya ajabu baada ya kukubali bao kurudi zote tatu na kufanya mabao kuwa 3-3. Liverpool sasa wanaingia kwenye Vita ya kimiujiza ili waweze kutwaa Ubingwa baada ya leo kuteleza vibaya. Ikiwa imebaki mechi yao moja tuu kumalizika kwa msimu wakiwa na mechi na Newcastle mtanange unaotarajiwa kuchezwa Jumapili 11. Sare hii pia inakuwa mbaya kwani pamoja na kuwa wapo juu kileleni wanatangulia kwa pointi moja tu juu ya Man City ambao wanauwezo wa kuwapita Jumatano kama wataweza kuifunga timu ya Aston Villa. Manchester City watakuwa Uwanjani kwao Etihad Jumatano Usiku kucheza kiporo chao na Aston Villa na wakitoka Sare au kushinda tu watatwaa tena uongozi na kuwa mbele ya Liverpool huku kila Timu ikiwa na Mechi 1 tu.3-2
Bao....1-0
Wachezaji wa Liverpool wakipongezana.Iconic: Suarez celebrates match Alan Shearer and Cristiano Ronaldo's record of 31 goals in a season3-0.....Suarez akibusu mkono wake baada ya kufunga baoLuis Suarez celebrates after scoring Liverpool's third at Palace.
Dakika ya 18 Liverpool wanapata bao la kwanza dhidi ya wenyeji Crystal Palace. Mfungaji akiwa ni Joe Allen dakika ya 18 baada ya Steven Gerrard kupiga kona na mabeki wa Crystal Palace kujichanganya na hatimaye Joe Allen kufunga bao kwa kichwa. Liverpool manager Brendan RodgersMpaka mapumziko Liverpool walikuwa wanaongoza kwa bao hilo 1-0 dhidi ya Crystal Palace. Kipindi cha pili dakika ya 53 Daniel Sturridge alifunga bao safi baada ya kupata pasi kutoka kwa Gerrard huku bao la tatu likifungwa na Luis Suarez katika dakika ya 55 baada ya kupewa pande na Raheem Sterling.Dwight Gayle celebrates after scoring his first goal against Liverpool.Dakika ya 79 Damien Delaney alifanya juhudi na kuweza kufunga bao la pili na kufanya 3-1 baada ya kupata pasi kutoka kwa Mile Jedinak na dakika moja baadae Crystal palace wakafunga bao la 2 na kufanya 3-2 kupitia kwa Dwight Gayle. Dakika ya 88 Crystal Palace wakapata bao la tatu na kufanya 3-3 kupitia kwa Dwight Gayle tena Glenn Murray akishinikiza kupatikana kwa bao hilo hilo!!Suarez akitupia bao la tatu na kufanya 3-02-0Hakunaga!!! Kipa hakuona ndani!!!Chezea mimi!!!kamata hii!! Rafu siyo dili hapa!!GerrardKamata mwizi!!Pata potea!!1-0 katika dakika ya 18 kipindi cha kwanzaMtajiju!!Furaha kwa wachezaji wa Liverpool mapema baada ya kupata bao la kwanza na hapa walikuwa wanapongezan......Mpaka ndaniMameneja wote pande zote mbili....Rogers na kocha wa Crystal palaceMeneja wa Liverpool
MSIMAMO ULIVYO KWA SASA TIMU ZA JUU:
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Liverpool
37
25
6
6
99
49
50
81
2
Man City
36
25
5
6
96
37
59
80
3
Chelsea
37
24
7
6
69
26
43
79
4
Arsenal
37
23
7
7
66
41
25
76
VIKOSI:
CRYSTAL PALACE
Speroni, Mariappa, Dann, Delaney, Ward, Dikgacoi, Jedinak, Ledley, Bolasie, Puncheon, Chamakh
Subs: Hennessey, Gabbidon, Parr, O'Keefe, Ince, Gayle, Murray
LIVERPOOL
Mignolet, Johnson, Flanagan, Skrtel, Sakho, Gerrard, Allen, Lucas, Sterling, Sturridge, Suarez
Subs: Jones, Toure, Agger, Coutinho, Aspas, Moses, Cissokho

Sunday, May 4, 2014


Vital: Dzeko (left) is congratulated by his team-mates after scoring the first of his goalsWakicheza Ugenini Goodison Park, Man City walitoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuifunga Everton Bao 3-2 na kutwaa Uongozi wa Ligi Kuu England kwa kuwakamata Liverpool kwa Pointi na wao kuongoza kwa ubora wa Magoli huku Mechi zimebaki 2 Ligi kwisha. Game over: The Manchester City players join Dzeko in celebration of his second goalDakika ya 11 kipindi cha kwanza Everton walipata bao kupitia kwa Barkley baada ya kupiga mpira kwenye umbali wa yadi 25 na kuzama mpaka nyavuni mwa lango la Manchester City.
Dakika ya 22 Aguero alisawazisha bao  kwa timu yake City na kufanya 1-1. Lakini muda kidogo aliumia na kulazimika kutolewa nje na nafasi yake ilichukuliwa na Fernandinho katika dakika 28.Aguero akichekiwa na docta wa timu kuona kama ataendelea au la!!

Edin Dzeko dakika ya 43 anaongeza bao la pili na kufanya 2-1 dhidi ya wenyeji Everton na mpira kwenda mapumziko City ikiwa mbele ya bao 1.
Dakika mbili kupita kutoka mpira uanze kipindi cha pili dakika ya 47 City wakapata bao la tatu lililofungwa na Edin Dzeko tena na akifanya 3-1.Nice one! City goalkeeper Hart celebrates team-mate Edin Dzeko scoring their third goal of the gameKipa wa City nae alishangilia bao hilo!Edin Dzeko
Everton hawakubweteka walitafuta bao na dakika ya 65 Lukaku aliwapachikia bao na kubadilisha matokeo kuwa 3-2.

Ushindi huu wa bao 3-2 City wamepanda kileleni wakiwa na pointi 80 wakilingana na Majogoo Liverpool wakitofautiana mabao ya kufunga.Joy: The Everton players join Barkley as the team celebrate his brilliant first half strikerKipigo hiki kimeondoa matumaini ya Everton kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu ujao na kuipa nafasi hiyo Arsenal.Bullet: Romelu Lukaku scored a brilliant diving header to give his side hope in the second halfLukaku akifunga bao la pili
Sasa City wamebakisha michezo miwili tuu nayo ni ya Nyumbani kwake Etihad msimu kumalizika, Timu hizo ni Aston Villa tarehe 7 mwezi huu wa tano na mechi ya mwisho ni tarehe 11 na watawakaribisha tena West Ham United.
michezo mingi kwa City itakuwa ya kujipima nayo itapigwa mwezi saba na wamepanga kucheza na Milan na Liverpool.


MABINGWA WATARAJIWA - MITANANGE WALIOBAKIWA NAYO!

CHELSEA
Mei 4: Chelsea v Norwich
Mei 11: Cardiff v Chelsea

LIVERPOOL 
Mei 5: Palace v Liverpool
Mei 11: Liverpool v Newcastle

MANCHESTER CITY 
Mei 7: City v Aston Villa
Mei 11: Man City v West  Ham United


Jubilant: Napoli's players celebrate with the Coppa Italia trophy after beating FiorentinaNapoli wameichapa Fiorentina Bao 3-1 na kutwaaTaji lao la 5 la Coppa Italia kwenye Fainali iliyochelewa kuanza kwa Dakika 45 kufuatia Mashabiki Watatu kupigwa risasi karibu ya Stadio Olimpico Mjini Rome, Italia ambako Fainali hiyo ilichezwa.
Let me hold it: Napoli hole the Coppa Italia trophy aloft after the win in Roma
Bao mbili za Mchezaji wa Kimataifa wa Italy, Lorenzo Insigne, ziliifanya Napoli iende Mapumziko ikiwa Bao 2-1 mbele huku Bao la Fiorentina likifungwa na Juan Manuel Vargas.
Double: Napoli's Lorenzo Insigne (second right) celebrates with his team-mates after scoring against Fiorentina
Dries Mertens aliifungia Napoli Bao la 3 katika Dakika za Majeruhi.
Napoli walimaliza Mechi hii wakiwa Mtu 10 baada Mchezaji wao Gokhan Inler kutolewa kwa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 79 baada ya kulambwa Kadi za Njano 2.

Main man: Insigne (left) scored twice during the Italian Cup final match at the Olympic Stadium
Mechi hii ilikuwa hatarini kufutwa kufuatia Mashabiki Watatu kupigwa risasi kutokana na vurugu za Mashabiki.
Proud: Napoli boss Rafa Benitez (left) spends some time with the trophy after the final whistle
Kocha wa Napoli, Rafa Benítez, aliongea baada ya Mechi: “Ilikuwa Mechi safi. Tulianza vyema lakini walipopata Bao lao na sisi kuwa Mtu 10 ilibidi tujikaze tushinde.
Controversial: Napoli fans threw flares onto the pitch before the match kicked-off
Hii ni mara ya 5 kwa Napoli kutwaa Coppa Italia na mara ya mwisho ni Mwaka 2012.

waliotembelea blog