Saturday, December 5, 2015

Man United baada  ya kukosa kukaa kileleni mwa Ligi Kuu England Wikiendi iliyopita walipotoka Sare ya 1-1 na Leicester City, sasa kazi kubwa kwa Man United Wikiendi hii ni kwanza kuhakikisha Rekodi yao ya kutofungwa Nyumbani kwao Old Trafford inadumu.Wakiwa ngomeni kwao Old Trafford, Man United wamefungwa Bao 1 tu Msimu huu na Jumamosi wanaivaa West Ham ambayo iko chini ya Kocha kutoka Croatia Slaven Bilic.
Hivi sasa Man United wako Nafasi ya 3 katika Ligi Kuu England wakiwa Pointi 1 nyuma ya Vinara Man City wanaofungana kwa Pointi na Leicester City.
MECHI YA LEO:
Licha ya kupata ugumu mkubwa wa kufunga Mabao, Man United wamekuwa wagumu kufungika ambapo hawajafungwa katika Mechi 6 za Ligi na hili limeisaidia kuwa juu kwenye Ligi.
West Ham wao wako Nafasi ya 8 baada ya kuanza vyema Ligi na hasa Mechi za Ugenini kwa kuzitwanga Arsenal, Liverpool na Manchester City lakini sasa hali imezorota na hawajashinda Mechi yeyote Mwezi wote wa Novemba na mara ya mwisho kushinda ni hapo Oktoba 24 walipokuwa kwao Upton Park na kuichapa Chelsea 2-1.

DONDOO MUHIMU:

-West Ham hawajashinda Old Trafford tangu Carlos Tevez alipofunga Bao la ushindi Msimu wa 2006/07 na kuwanusuru kushuka Daraja.
-Tangu wakati huo, Mechi zote 7 za Ligi zilizochezwa Old Trafford, Man United wameshinda.

WACHEZAJI:

Man United itawakosa Kepteni Wayne Rooney, Phil Jones, Marcos Rojo na Ander Herrera ambao ni Majeruhi wakiungana na wale wa muda mrefu Antonio Valencia na Luke Shaw.
West Ham itawakosa Majeruhi Dimitri Payet, ambae ndie Mfungaji wao Bora, Straika wao hatari Diafra Sakho pamoja na Enner Valencia.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog