Diamond akiangalia vipande vya video hivyo kabla ya kuendelea kushuti.
Sasa hivi kwenye ulimwengu wa muziki, gumzo ni ngoma aliyoitoa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ inayokwenda kwa jina la Utanipenda. Ni ngoma kali ambayo itatambulishwa kwa mara ya kwanza ndani ya Ukumbi wa Kimataifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar.
Mbali
na utambulisho wa ngoma hii ambayo itapigwa live kwa kutumia vyombo,
nyimbo nyingine ambazo Diamond atazipiga siku hiyo ni pamoja na
Mdogomdogo, Nasema Nawe, Nana na nyinginezo zinazobamba huku akiwa na
madansa wake kutoka Wasafi Classic Baby (WCB). Itakuwa ni siku ya
Krismasi (Ijumaaa ijayo) ambayo msanii huyo ameahidi kufanya mambo
makubwa akisindikizwa na mkali wa nyimbo za Singeli, Msaga Sumu pamoja
na wacheza dansi hatari Afrika Mashariki, Wakali Dancers na wasanii
wengine kibao.
Burudani
yote hiyo ambayo imedhaminiwa na huduma kutoka kampuni ya simu
Tanzania, Airtel Money utaipata kwa kiingilio cha shilingi 15,000 tu
getini na wale watakaohitaji huduma ya VIP watalipia shilingi 30,000.
Katika kuelekea kwenye shoo hiyo, Showbiz ilifanikiwa kunasa baadhi ya
picha za nyuma ya pazia ‘behind the scene’ wakati kichupa cha wimbo huo
kikiandaliwa.
0 maoni:
Post a Comment