Diamond
Platnumz akiwasalimia mashabiki wake waliofurika katika eneo la Karume
leo kwenye mkutano na wanahabari kuhusu shoo yake itakayofanyika Dar
Live kwenye Sikukuu ya Krismasi.
Diamond akiimba wimbo wake mpya wa Utanipenda sambamba na mashabiki waliofurika Karume leo.
Mashabiki wakiwa wamepagawa wakati Diamond akiimba wimbo wake mpya wa Utanipenda.
Meneja
Masoko wa Global Publishers na Dar Live, Innocent Mafuru (mwenye
tisheti nyeupe aliyesimama kulia) akiwakaribisha wanahabari, wasanii na
mashabiki wa burudani katika mkutano na wanahabari kuelekea shoo ya
Funga Mwaka itakayofanyika Dar Live kwenye Sikukuu ya Krismasi.
Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho akielezea jinsi walivyojipanga kwa shoo hiyo ya Krismasi.
Meneja
Uhusiano Msaidizi wa Airtel Tanzania, Jane Matinde akionyesha kadi ya
Airtel Money Tap Tap inayomuwezesha mteja kufanya malipo mahali popote
na watakaohudhuria shoo ya Diamond kununua tiketi kwa punguzo la
shilingi 5000 kwa wateja 1000 wa kwanza.
Mratibu
wa Burudani Dar Live, Juma Mbizo akiongea na wanahabari pamoja na
mashabiki (hawapo pichani) kuhusu walivyojipanga kuwapa burudani
mashabiki siku ya Krismasi.
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Staric ambaye naye atapanda jukwaani siku hiyo akiongea na mashabiki.
Diamond akizidi kuwapagawisha mashabiki wake.
Baada ya kuongea na mashabiki wake Diamond aliamua kugawa CD na DVD za nyimbo zake kwa mashabiki waliohudhuria.
Diamond akiwaaga mashabiki na kuwataka wakutane Dar Live katika Sikukuu ya Krismasi.
Mashabiki wakiwa wamemzingira Diamond wakati akiondoka eneo la mkutano na wanahabari leo.
STAA
wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewaahidi shoo ya
nguvu mashabiki wake na kuwataka waje kwa wingi katika shoo kali ya
kufunga mwaka itakayopigwa Dar Live, Mbagala Zakhem, Dar katika Sikukuu
ya X-mas na kuwa hatawaangusha.
Diamond anayetamba na ngoma ya Utanipenda ameyaongea hayo leo kwenye
mkutano maalum uliofanyika Karume, Dar ambao ulihusisha waandishi wa
habari na wapenzi wa muziki kwa ajili ya kuzungumzia shoo hiyo kubwa
kuliko inayojulikana kama Funga Mwaka Concert.
“Itakuwa ni Sikukuu ya Krismasi, sasa kwa nini tusifurahi pamoja, kama
MTV wameamua kunipa tuzo ya Mtumbuizaji Bora Afrika kwa hiyo sihitaji
kuongea sana shoo itakuwaje siku hiyo, naomba mje kwa wingi kwa kweli
sipendi kuwaudhi, nawaahidi sitawaangusha,” alisema Diamond au Baba
Tiffah.
Pia waandaji wakuu wa shoo hiyo, Global Publishers Ltd, kupitia kwa
Meneja Mkuu, Abdallah Mrisho, naye alizungumza machache pamoja na
kutambulisha listi ya wasanii wengine watakaoambatana na Diamond siku
hiyo.
“Mbali na Diamond pia kutakuwa na Msagasumu, Wakali Dancers, Staric
pamoja na burudani nyingine nyingi.
Haitakuwa shoo ndogo, Diamond ameamua kufurahi na mashabiki wa muziki
siku ya Krismasi kwa kufunga na kuukaribisha mwaka mpya. Shoo zitaanza
asubuhi kwa watoto mpaka saa 12 jioni kisha baada ya hapo ni watu wazima
mpaka alfajiri,” alisema Mrisho.
Viingilio ni Sh 15,000 na kwa V.I.P ni Sh 30,000 lakini wadhamini wakuu
wa shoo hiyo, Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel wakaamua kutoa ofa ya
punguzo la bei kwa tiketi 1,000 za awali kwa watakaokata kupitia kadi
mpya za Airtel Money Tap Tap zenye mfumo mpya wa kulipia bili
mbalimbali.
“Kadi za Tap Tap zinazorahisisha kufanya malipo zaidi popote ulipo bila
ya gharama yoyote tayari zipo zinapatikana maeneo ya Temeke na Ilala
lakini kuwa nayo unapaswa kuwa na kadi ya Airtel na kwa wateja 1,000 wa
kwanza wenye Tap Tap watakaokata tiketi kupitia kadi hiyo watakuwa na
punguzo la Sh 5,000 yaani kwa 15,000 itakuwa 10,000 na 30,000 itakuwa
25,000,” alisema Meneja Uhusiano Msaidizi wa Airtel Tanzania, Jane
Matinde.
Habari: Hans Mloli,
0 maoni:
Post a Comment