USIKU WA EUROPA LEO – TIMU KUTAFUTA POINTI MUHIMU, NANI KUFUZU, NANI KUFELI?
Borussia Dortmund, Napoli, Rapid Wien na Braga ni miongoni mwa Timu zinazoweza kufuzu Usiku huu huku wakibakisha Mechi 2 mkononi za Makundi yao.
Leo zinachezwa Mechi za 4 za Makundi na Timu 9 kati ya 48 zinaweza kufuzu hii Leo wakati Timu 5 zinaweza kutupwa nje ya Mashindano hayo hii Leo.
IFUATAYO NI TATHMINI TOKA KILA KUNDI:
Kwenye Mabango ni Pointi za Timu.
KUNDI A:
Celtic (2) v Molde (7)
Ajax (2) v Fenerbahçe (4)
-Ikiwa Molde watashinda na Ajax hawashindi, Molde watafuzu.
KUNDI B:
Rubin (2) v Liverpool (3)
Sion (7) v Bordeaux (2)
-Sion wakishinda wamefuzu.
KUNDI C:
Krasnodar (4) v PAOK (3)
Borussia Dortmund (7) v Qäbälä (1)
-Ikiwa Dortmund na Krasnodar watashinda, basi Dortmund watafuzu.
KUNDI D:
Club Brugge (1) v Legia Warszawa (1)
Napoli (9) v Midtjylland (6)
-Ikiwa Napoli watashinda, wamefuzu.
-Ikiwa Brugge v Legia ni Sare, Napoli wamepita.
-Ikiwa Midtjylland watashinda na Gemu nyingine Sare, wote Napoli na Midtjylland watafuzu
-Ikiwa Midtjylland watashinda, basi kipigo kwa Brugge au Legia kitamtupa nje aliefungwa.
KUNDI E:
Dinamo Minsk (0) v Villarreal (6)
Viktoria Plzeň (3) v Rapid Wien (9)
-Ikiwa Rapid watashinda, watafuzu.
-Ikiwa Dinamo watafungwa, watatupwa nje.
KUNDI F:
Marseille (3) v Braga (9)
Groningen (1) v Slovan Liberec (4)
-Ikiwa Braga watashinda, watafuzu.
KUNDI G:
Rosenborg (1) v Lazio (7)
Saint-Étienne (4) v Dnipro Dnipropetrovsk (4)
Kundi lipo wazi.
KUNDI H:
Beşiktaş (5) v Lokomotiv Moskva (7)
Skënderbeu (0) v Sporting CP (4)
-Ikiwa Lokomotiv watashinda na Sporting hawashindi, basi Lokomotiv watafuzu.
-Ikiwa Skënderbeu wtafungwa basi wako nje.
KUNDI I:
Belenenses (4) v Basel (6),
Lech Poznań (4) v Fiorentina (3)
-Kundi lipo wazi.
KUNDI J:
Qarabağ (3) v Monaco (5),
Tottenham Hotspur (4) v Anderlecht (4)
-Kundi lipo wazi.
KUNDI K:
Sparta Praha (5) v Schalke (7)
Asteras Tripolis (1) v APOEL (3)
-Ikiwa Schalke watashinda, watafuzu.
KUNDI L:
Augsburg (3) v AZ Alkmaar (3)
Athletic Club (6) v Partizan (6)
-Kundi lipo wazi.
0 maoni:
Post a Comment