Friday, November 13, 2015



Kuelekea michuano ya mataifa ya Ulaya yatakayofanyika mwaka 2016, shirikisho la soka barani Ulaya limetangaza mpira maalum kwa ajili ya kutumika katika mashindano hayo, mpira wa utaotumika katika mashindano hayo ya mataifa ya Ulaya kwa mwaka 2016 umetengenezwa na kampuni ya vifaa vya michezo ya kijerumani ADIDAS.
2E5E9C7500000578-0-image-a-42_1447327190930
Mpira huo maalum wa Euro unaoitwa kwa jina la kifaransa la ‘Beau Jeu’ ambapo kwa kiingereza unatafsiriwa kwa jina la ‘the beautiful game’ unatajwa kufanana na mpira (Brazuca) uliotumika katika michuano ya Kombe la Dunia 2014 iliyofanyika Brazil . Mpira wa ‘Beau Jeu’ ulitengenezwa kwa zaidi ya miezi 18.
Michuano ya Euro 2016 itafafanyika Ufaransa lakini ADIDAS imekuwa ikipokea tenda ya kutengeneza mipira ya mashindano hayo kwa miaka mingi sasa.
download (2)
Hii ni List ya mipira ya Euro iliyokuwa inatumika kuanzia mwaka 1960 hadi utakaotumika mwaka 2016
1E7EDE1B00000578-3315271-image-a-53_1447328424468
Huu ni mpira wa Brazuca ambo ulitumika mwaka 2014 katika michuano ya Kombe la Dunia Brazil ila unatajwa kufanana na wa Euro 2016

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog