Mchezo wa mpira wa miguu ni miongoni mwa
kazi zinazotajwa kulipa mishahara mikubwa zaidi duniani, siku hizi
imekuwa kawaida kusikia mchezaji huyu na yule kuwa na mshahara wenye
tofauti kubwa. Kwa sasa Ligi Kuu soka Tanzania bara inatajwa kuwa ni moja kati ya Ligi zinazoongoza kwa kulipa mishahara mikubwa tofauti na baadhi ya Ligi za nchi jirani.
November 9 nakusogezea karibu yako sehemu ya exclusive interview ya Henry Joseph ambapo amezungumza kuhusiana na mishahara na jinsi alivyoingia Simba. Henry aliingia Simba mwaka 2006 baada ya kumaliza kidato cha nne ilikuwaje? mkataba wake je? mshahara wake?
“Ilitokea
tu kama bahati nikaitwa na mwenyekiti wa Simba alikuwa Wambura wakati
ule na kocha Julio nikacheza mechi ya majaribio, baadae nikapigiwa simu,
Nikapewa mkataba wa miaka miwili nikasaini hata bila kuusoma Simba
tena, mshahara wakati huo bwana wachezaji wote tulikuwa tunalipwa sawa
laki moja na ishirini tofauti na siku hizi” >>> Henry Joseph
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Henry Joseph ni kiungo wa zamani wa klabu ya Simba na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars lakini amewahi kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Kongsvinger ya Norway ila kwa sasa yupo katika klabu ya Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani.
0 maoni:
Post a Comment